Na Augustine Mgendi, BUTIAMA
WATANZANIA
wametakiwa
kuchukia vitendo vya rushwa,ubaguzi,ukabila,udini na ubinafsi
ili kulinda amani ya nchi ikiwa ni njia moja wapo ya kumuenzi kwa
vitendo baba
wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kabarage Nyerere.
Hayo
yamesemwa
kijijini Butiama mkoani Mara na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru
kitaifa
mwaka huu Bw Honest Ernest Mwanonossa,mbele ya kaburi la baba wa taifa,
baada
ya kuwasha Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa baba wa taifa hayati mwalimu
Julius
Kambarage Nyerere katika eneo la Mwitongo.
Amesema
kuna
baadhi ya viongozi nchini wameshindwa kumuenzi Baba wa taifa kwa kukemea
kwa
vitendo matumizi ya ukabila,udini na rushwa hasa katika siasa jambo
ambalo ni hatari na kwamba vitendo hivyo visipothibitiwa mapema vinaweza
kuhatarisha amani ya nchi.
Akiwa
kijijini
Butiama, kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa,ameweka jiwe la msingi
katika jengo la wodi ya wazazi na watoto ambalo linajengwa kwa
ushirikiano wa
wananchi wa kijiji cha Butiama,Halmashauri ya Musoma vijijini na
Serikali
kuu kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 483 kama sehemu ya kuongeza
miundo
mbinu katika hospitali hiyo inayotarajiwa kuwa ya wilaya mpya ya
butiama.
Awali
viongozi
hao wakiongozwa na kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitafa,wamepata
fursa
ya kuomba na kuweka mashada ya maua katika kaburi la baba wa taifa
hayati
mwalimu Julius Nyerere.
