UZALISHAJI WA UMEME KATIKA BWAWA LA MUNGU UPO HATARINI KUSITISHWA

 Bwawa la nyumba ya Mungu

Na Belinda Semtandi, MOSHI

BODI ya maji bonde la pangani imesema kufuatia  hali ya maji katika bwawa la nyumba ya mungu kupungua sana kutokana na kukosekana na kwa mvua za masika na uharibifu wa mazingira uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo uko hatarini kusitishwa

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa bodi ya maji bonde la pangani Julius sarmatt wakati wa mkutano wa wadau wa maji kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini waliokutana mjini moshi na kueleza kuwa hali ya bwawa hilo kwa sasa ni mbaya

Alisema kiwango cha uzalishaji umeme katika bwawa hilo umeshuka kutoka megawati 8 zilizokuwa zinazalishwa awali hadi kufikia megawatt 3 hali ambayo  ni hatari  na  kwamba endapo hali hiyo itaendelea itasababisha mitambo ya umeme katika bwawa hilo kushindwa kuzalisha umeme

Aidha mwenyekiti huyo aliongeza kuwa  upungufu uliojitokeza mwaka huu haujawahi kutokea katika kipindi cha miaka ya nyuma na kwamba walitegemea endapo mvua za masika zingenyesha vizuri kungesaidia kuongeza maji katika bwawa hilo bila mafanikio za kwamba maji yanzidi kupungua siku hadi siku.

“ kutokana na upungufu huo tumeanzisha mpango wa mkakati wa kuelimisha wananchi juu ya kuanzisha vyama vya usimamizi wa maji na kulinda vyanzo vya maji hatua ambazo zitaweza kupunguza tatizo la maji katika bwawa hilo”alisema sarmatt

Mapema akizungumza na wadau wa maji kutokoka mikoa ya arusha ,Kilimanjaro,manyara,tanga waliokutana mjini moshi kujadili utekelezaji wa mpango wa miaka 25 wa usimamizi na endelezaji wa raslimali za maji katika bonde la pangani katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Faisali Issa alisema kuwa hali ya  maji kwa mkoa wa Kilimanjaro ni mbaya

Kutokana na hali hiyo Issa aliwataka wenye viwanda na mashamba makubwa ya umwagiliji kuangalia uwezekano wa kupunguza matumizi ya maji yasiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na kusafisha maji taka ili kurudi katika mzunguko hali ambayo itapunguza tatizo la ukosefu wa maji ambao umesababisha kuwepo kwa migogoro baina ya wananchi waishio ukanda wa juu na wale waishio ukanda wa chini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo