Mawaziri wa Masuala ya
Usalama katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
wamepitisha
bila kupinga, Uganda kuwa mwenyeji wa Kituo cha Rufaa cha Kuchunguza
Vielelezo
vya Uhalifu (RFRC) vinavyohitajika katika kesi mbalimbali kwenye
mahakama ndani
ya kanda.
Azimio hilo lilipitishwa mjini Kigali katika kikao
cha siku
moja kilichomalizika Jumatatu.
Hata hivyo, uamuzi huo unatakiwa kuthibitishwa na
Baraza la
Sekta ya Usalama linalojumuisha mawaziri wanaohusika na mambo ya ndani,
shughuli za maafa, uhamiaji, polisi, magereza, intelijensia na udhibiti
wa
ugaidi.
Uamuzi wa umuhimu wa kupata kituo cha rRFRC
ulifikiwa
katika mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi katika nchi
tano
wanachama mjini Kigali uliomailizika Ijumaa iliyopita.
Wakuu hao wa majeshi ya polisi waliunga mkono hatua
hiyo
baada ya kuzingatia taarifa ya utafiti ya ujumbe wa EAC uliotembelea
nchi zote
tano wanachama Machi mwaka huu.
Pia walizingatia taarifa ya kina ya uchunguzi huru
wa
mshauri wa uchunguzi wa vielelezo vinavyohitajika mahakamani kutoka
Uingereza
aliyekodiwa na EAC-GIZ na alishiriki katika ujumbe wa uthamini akiwa na
wataalamu wa uchunguzi huo kutoka nchi za EAC.
Katibu Mkuu wa EAC, Dk Richard Sezibera alisisitiza
wakati
akifungua mkutano wa mawaziri Jumatatu umuhimu wa ulinzi na usalama
katika
kanda.
‘’ Wananchi Afrika Mashariki, mmoja mmoja na kwa
ujumla wao
wanategemea usalama wao kuimarika kwa vile utaratibu wa utangamano
unaendelea
kukua,’’ aliwaambia wajumbe.
Aliongeza: ‘’Mategemeo ni kwamba tishio la ugaidi,
usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya pamoja na matishio
mengine
ya usalama yatadhibitiwa vyema na kwa njia rahisi,’’ Dk Sezibera
alinukuliwa
akisema, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EAC kwa waandishi wa
habari.
Katibu huyo Mkuu wa EAC pia aliwapongeza Wakuu wa
Majeshi
ya Polisi kwa uamuzi wao kuanzisha kituo hicho cha rufaa cha uchunguzi.
Mwanyekiti wa Mkutano huo, Beatrice Kones kutoka
Kenya
alisema kuna haja kwa kanda kuwa na juhudi za pamoja kushughulikia
tishio
lolote la kiusalama.
‘’Bila amani, hakuna usalama na bila usalama hakuna
maendeleo,” Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya aliliambia Shirika
Huru la
Habari la Afrika Mashariki (EANA) nje ya mkutano huo.
Alisema pia kuwa RFRC itaanza shuguli zake muda
mfupi ujao.
Serikali ya Ujerumani imeonyesha nia ya dhati
kuunga mkono
uanzishwaji wa RFRC wa kisasa.