Ikiwa imebaki Siku moja kuanza kwa zoezi
la Sensa ya Watu na Makazi kwa nchi nzima baadhi ya Viongozi wa Dini ya
Kislam kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu waliokuwa wakipinga zoezi
hilo wamejiengua katika Jumuiya na Taasisi hizo na kuungana na
Watanzania wengine kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Taasisi ya Islamic Peace Foundation, Sheikh SADIKI
GODIGODI amevitaka Vyama vya siasa nchini kuacha tabia ya kuwatumia
baadhi ya Viongozi wa dini kuanzisha migogoro na Serikali likiwemo suala
la kuwashawishi waumini wa Dini ya kiislam kutoshiriki zoezi la Sensa
ya Watu na Makazi.
Katika hatua nyingine Sheikh GODIGODI
ameeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya Watu kusambaza ujumbe wa simu
kwa Waumini wa Dini ya kiislam ukiwataka kutoshiri zoezi hilo na
kuwataka Waislam kote nchini kupuuza ujumbe huo na kuwataka kushiriki
ipasavyo katika Sensa ya Watu na Makazi kwani ni haki yao.
Kwa upande wake mmoja wa Wahadhiri
aliyejiengua kutoka kwenye Jumuiya na Taasisi za kiislam ambao
wanapingana na zoezi hilo, amesema kwamba amifikia uamuzi wa kujitoa
katika Jumuiya hiyo kutokana na kutoona mantiki ya kupinga zoezi la
Sensa ya Watu na Makazi kutokana na umuhimu wake katika utekelezaaji wa
maendeleo nchini.
