Na Belinda Semtandi, Arusha
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa Dk. Julius Rotich
ametaka kuwepo kwa juhudi za pamoja kudhibiti wahalifu ambao
‘’wanaonekana
kuleta shirikisho kati yao kwa haraka zaidi kuliko nchi wanachama .’’
Alisema viwango vya uhalifu kwa kutumia
mbinu
za kisasa unazidi kuongezeka kutokana na nafasi nyingi za kujipatia
elimu huku
kukiwa na tatizo la ukosefu wa ajira.
‘’Changamoto hii inawataka nyinyi
wapelelezi kwendana
na hali ya kuwa tayari kukabiliana nayo kwa kuimarisha uwezo wa
upelelezi ili
kujihakikishia kwamba wahalifu wanatiwa hatiani,’’ alisema.
Dk. Rotich alikuwa anahutubia mkutano
wa
Wakurungenzi wa Upelelezi, Wasajili wa Magari na Wakuu wa Vitengo vya
Kupambana
na Madawa ya Kulevya na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, mjini Nairobi,
Kenya,
mwishoni mwa wiki.
Alifafanua kwamba mahitaji ya hali ya
juu ya
haki za binadamu na uwasilishaji wa ushahidi ndani ya kanda hiyo
umeongeza
shinikizo zaidi la kuwepo na nia ya kuimarisha uwezo wa kiufundi katika
suala
zima la upelelezi.
Ni kutokana na umuhimu huo basi,
Sekretarieti
ya EAC imeweka kipaumbele katika kuanzisha kituo cha uchunguzi cha
kanda.
Alielezea masikitiko yake kuhusu
taarifa za
wataalamu kwamba wasafirishaji wa madawa ya kulevya pamoja na
usafirishaji
haramu wa binadamu wanatumia kanda ya Afrika Mashariki kama njia yao
kuuu ya
kupitisha uhalifu huo.
Naye Mkuu wa ujumbe wa Tanzania katika
mkutano
huo, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Peter Kivuyo amezitaka nchi wanachama
kutoa
adhabu kali zaidi kwa wahalifu wa madawa ya kulevya.
‘’Hivi sasa adhabu zinazotolewa kwa
wahalifu wa
madawa ya kulevya au mawakala wao siyo kali vya kutosha kuweza
kuwaogopesha
watu wengine kutothubutu kujiingiza katika biashara hiyo,’’ alisisitiza.
Akizungumza katika mkutano huo pia,
Mkuu wa
Upelelezi nchini Rwanda, Christopher Bizimungu alisema ushirikiano wa
ubadilishanaji wa taarifa za kiintelejensia katika EAC zimesaidia
kuwatia
mbaroni wahalifu wa madawa ya kulevya.
‘’Ushirikiano miongoni mwa nchi
wanachama wa
EAC umeleta mafanikio katika kudhibiti uhalifu wa madawa ya kulevya
katika
kanda yetu.’’
