Imebainishwa
kuwa ugonjwa wa Trakoma ni moja ya adha kubwa inayosumbua jamii ya
watanzania
hasa waishio vijijini katika mazingira yasiyoridhisha kwa usafi na
ukosekanaji
wa maji.
Hayo
yamebainishwa na mganga mkuu wa mkoa wa manyara Dr Samuel Ulomi wakati
alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya utafiti wa awali wa
ugonjwa
wa Trakoma jana ya siku nne katika ukumbi wa Veta mkoani Manyara.
Alibainisha
kuwa ugonjwa wa Trakoma umegundulika kuathiri sana wakinamama pamoja na
watoto walio na umri wa miaka kati ya mwaka mmoja hadi miaka kumi,
pamoja na
adha ya ugonjwa huo kwa rika hilo watoto,trakoma ni moja ya
magonjwayaletwayo
upofu katika umri wa miaka 15-60 na zaidi.
Dr
Ulomi alifafanua kuwa baada ya utafiti huo lengo ni kuanza mikakati
ya udhibiti wa ugonjwa wa Trakoma kwa kutumia mikakati ya usafi katika
wilaya
zote zitakazogundulika kuwa na ugonjwa kwa kiwango cha zaidi ya asilimia
10%.
Naye
mratibu waTaifa wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka wizara ya Afya
Dr
Upendo Mwingira alieleza kuwa kutokana na hali hiyo shirika la Afya
duniani
lilipitisha azimio la kutokomeza upofu unaotokana na Trakoma duniani
kote
ifikapo mwaka 2020,liliundwa mwaka 1999 linaitwa Global elimination of
Trakoma
by the year 2020.
Aliongeza
kuwa wizara ya Afya na stawi wa jamii,jamuhuri ya muungano ya Tanzania
iliridhia azimio hilo la shirika la afya ulimwenguni na kupanga mikakati
mbalimbali ya udhibiti wa ugonjwa wa Trakoma nchini.
Aidha
alisema kuwa kwa ushirikiano na shirika la International Trakoma
initiative(ITI)katika miaka ya 2004-2006 ulifanyika utafiti wa awali wa
ugonjwa
wa Trakoma katika wilaya 50 ambazo ziligundulika kuwa ugonjwa huo kwa
viwango
mbalimbali na mikakati ya udhibiti wa ugonjwa huo.
Kwa
upande wake meneja wa mradi wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
mabusha,matende,vikope,trakoma,kichocho,minyoo ya tumbo,usubi kutoka
shirika
lisilo la kiserikali(NGO)IMA world health Dr Deogratias Damas
alisisitiza kuwa hadi kufikia mwaka 2012 jumla ya mikoa 13 zinatekeleza
mpango
huo NTD hapa nchini.
Alisema
kuwa katika mpango mkakati wa miaka mitano wa NTD moja ya kipaumbele ni
kukamilisha utafiti wa awali katika wilaya ambazo hazikufanyiwa utafiti
na kwa
mwaka huu wizara,wadau wanatekeleza kazi hii ya tathmini ya awali katika
wilaya
10 na pia utafiti wa ufuatiliaji katika wilaya tatu.
Katika
mafunzo hayo washiriki ni kutoka wilaya Babati pamoja na wilaya ya
Mbulu
wizara ya afya imeshirikisha wilaya hizi katika utafiti huo wa awali wa
ugonjwa
wa Trakoma na mada zilizotolewa ni vikope lengo mkakati wa kupambana na
ugonjwa
wa vikope malengo ya kuangalia kiwango cha maambukizi ,namna ya kufanya
utafiti
kwa kuangalia ugonjwa wa vikope.
