VIONGOZI
wa
Kanisa Katoliki jimbo la Musoma katika Parokia za Ingiri wilayani Rorya
na
Nyamwaga wilayani Tarime mkoani Mara,wameishauri serikali kutumia
raslmali za
ndani yakiwemo madini katika kuongeza mapato ya nchi badala ya kutegemea
misaada ya wahisani.
Wamesema
hatua
hiyo italiwezesha taifa kuwa na mapato yake ya uhakika ambayo
yatachangia kwa
kiasi kikubwa kuharakisha maendeleo ya wananchi katika utekelezaji wa
miradi mingi ya maendeleo.
Wakizungumza
katika
ibada maalum ya mavuno katika kuelekea Jubilii ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa parokia ya Ingiri,viongozi hao wa kanisa
Katoliki,wamesema kuwa
hata Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere katika uhai wake
alisimamia
na kulinda raslimali za nchi kwaajili ya watanzania ingawa hivi sasa
hali
ni tofauti kutokana na raslimali hizo kutowanufaisha wananchi.
Naye
mgeni rasmi
katika ibada hiyo maalum,mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mh Vicent
Nyerere,ametumia nafasi hiyo kuwaambia waumini wa kanisa hilo, kuwa
pamoja na
nia njema ya serikali ya kukubali kuanzisha mchakato kuandikwa kwa
katiba
mpya,lakini kuna hatari kwa kupatikana kwa katiba ambayo haitakidhi
mahitaji ya
watanzania kutokana na wananchi walio wengi kushindwa kujitokeza kutoa
maoni
mbele ya tume ambayo imeundwa na rais.
Katika
ibada
hiyo ambayo imewezesha kupatikana kwa magunia 11 ya nafaka na ndoo sita
za
rangi,viongozi wa kanisa hilo wametumia misa hiyo kusisitiza somo la
uwajibikaji na kufanya kazi kwa bidii kama njia moja wapo ya kupambana
na
umasikini.
