SERENGETI
Mkazi
mmoja wa
kijiji cha Gentamome wilayani Serengeti mkoani Mara, amejeruhiwa vibaya
katika sehemu
mbalimbali za mwili wake baada ya kushambuliwa na fisi aliyevamia
nyumbani
kwake.
Mwenyekiti
wa
serikali ya kijiji hicho cha Gentamome Bw Elisha Sinda,amesema kuwa
tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia Agosti tisa mwaka huu.
Amemtaja
mwananchi
huyo kuwa ni Bw Juma Kurate ambaye mbali na kujeruhiwa katika sehemu
hizo za mwili wake pia fisi hiyo alimnyofoa kidore gumba cha mkono wake
wa
kushoto.
Bw
Sinda,amesema
baada ya fisi huyo kuvamia nyumbani kwa mwananchi huyo kwa lengo la
kukamata
mbuzi ndipo walipopambana na makazi huyo kabla ya kumjeruhi na kukimbia
na
kidore hicho kabla ya kuuawa katika msako mkali uliofanywa na wananchi
wa
kijiji hicho.
Kwa
sababu hiyo
mwenyekiti huyo wa kijiji,ameiomba idara ya wanyamapori wilayani
Serengeti
kuendesha msako dhidi ya fisi hao ambao amesema wamekuwa kero kubwa kwa
wananchi kutokana na kupora kila wakati mifugo ya wananchi lakini licha
ya
kutoa taarifa katika idara hiyo hakuna hatua ambazo zimechukuliwa.