MTOTO WA MWAKA MMOJA AUAWA NA BABA YAKE MZAZI

 
Dinna Maningo,Tarime.

MTOTO mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja ameuwawa baada ya kupigwa fimbo kichwani na baba yake mzazi Migengo Mseti (68) Mkazi wa Kijiji cha Nyakunguru kata ya Kibasuka Wilayani Tarime.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo nakwamba lilitokea Agosti 8 majira ya saa 10.30 jioni kitongoji cha Turuturu kijiji cha Nyakunguru ambapo mtoto aitwaye Buyuri Mseti aliuwawa.

Kamanda Kamugisha alisema kupigwa kwa mtoto huyo kulitokana na sababu za ugomvi kati ya baba na mama yake Magreti wakati baba huyo akimpiga mke wake alikuwa amebeba mtoto mgongoni na kwamba wakati baba akijaribu kumpiga mke wake kwa fimbo mama huyo alikwepa fimbo na ndipo ilipompata mtoto Kichwani na kumsababishia kifo papo hapo.

Kamugisha aliongeza kuwa mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi tayali kwa mazishi nakwamba mtuhumiwa amekamatwa na yuko chini ya ulinzi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo