SINGIDA
Serikali imeahidi
kuvipatia umeme wa grid vijiji 21 vya jimbo la Iramba Magharibi na
Iramba
Mashariki ili pamoja na mambo mengine kuharakisha upatikaji wa maendeleo
endelevu.
Akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Kaselya jimbo la Iramba Magharibi Naibu Waziri wa
Nishati na Madini George Simbachawene, amesema kati ya vijiji hivyo,
kijiji cha
Msingi na Milade, ni vya jimbo la Iramba Mashariki na vilivyobaki 19 ni
vya
jimbo la Iramba Magharibi.
Simbachawene ametaja
baadhi ya vijiji vya jimbo la Iramba Magharibi vitakavyonufaika na mradi
huo
kuwa ni Kaselya, Mbelekese, Ndulungu, Malendi, Kitusha, Lugwala, Moto
moto,
Kizaga, Kitukuntu, Kibigiri, New Kiomboi, Makunda na Maluga.
Naibu Waziri huyo amesema
vijiji hivyo vitapata umeme kwa awamu tofauti, lakini vijiji vya
Mbelekese,
Kaselya na Ndulungu, vitapata umeme katika mwaka huu wa fedha
utakaoishia juni
mwakani.
Amesema kutokana na
hatua hiyo, hivi sasa hakuna haja ya vijana kukimbilia mijini ambako
hakuna
kazi za kufanya.
Naye mbunge wa jimbo
la Iramba Magharibi Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka wakazi wa maeneo
yatakayopatiwa umeme, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makandarasi
watakaopewa
kazi ya kusambaza umeme vijijini ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa
haraka.
.jpg)
