JESHI LA POLISI MKOANI KILIMANJARO KUIMARISHA DORIA MSIMUU HUU WA SIKUKUU YA ID ELFITR


Jeshi la Polisi Wilayani Siha Mkoani Kilamanjaro litafanya doria ya kukabiliana na vitendo vya kialifu katika maeneo mbalimbali Wilayani humo wakati wa shamra shamra za sikukuu ya Id ELFITIR

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo mkuu wa kituo cha polisi Wilaya Siha OCD SP LUTSIYA MWAKYUSA amesema kuwa Jeshi lake limejipanga kukabiliana na vitendo vya uvunjaji wa amani

Bw Mwakyusa amesema ili kudhibiti uhalifu wataimarisha doria Wilaya nzima kwa kushirikiana Polisi jamii ulinzi shirikishi ili kusitokee vurugu au vitendo vya uvunjifu wa amani hivyo amewaomba Wananchi kuwapa ushirikiano hili kutekeleza jambo hilo

Pia amesema vikosi vya usalama barabarani navyo vitawekwe katika hali ya tahazari kwani baadhi ya madereva hukiuka sheria kwa kuendesha magari wakiwa wamelewa hali ambayo inaweza ikachangia kutoakea kwa ajali

Katika hatua nyingine watu wasio julukana idadi yao wamevunja na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo simu akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa wa Sanya juu  Wema Gasino amesema tukio hilo limetokea agost 16 mwaka huu nyakati za usiku 

Amesema kuwa watu wasiojulikana idadi yao ambao wanasadikiwa ni vibaka walivamia dukani kwa bw Himanueli Masakuu  mkazi wa Sanya na kuiba simu na Loptop zenyethani ya sh milioni tisa na nusu pamja na vitu vingine ambavya havijajulikana idadi yake ,ambapo Polisi wa kituo cha Sanya juu wanaendelea na uchunguzi ilikubainini ni nani waliousika na tukio hilo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo