Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
DODOMA IJUMAA
AGOSTI 17, 2012. Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Jamuhuri John, mwenye umri wa miaka (28) amekutwa amejinyonga katika mti wa mbuyu baada ya
kuwajeruhi
kwa Panga mke na mtoto wake kisha kukimbia kusikojulikana.
Akizungumzia tukio
hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Edmundi Urio alisema
tukio hilo la kujinyonga liligundulika
mnamo tarehe 17/08/2012 majira ya saa 06:45 asubuhi, na wananchi
waliokuwa
wakimfuatilia katika Kijiji cha Kikombo Kata na tarafa ya Kikombo Wilaya
ya
Dodoma Mjini.
“Uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa chanzo cha
kujinyonga kwa mtu huyo ni ugomvi wa mapenzi kwani marehemu alikuwa
amewajeruhi
mke na mtoto wake kwa kuwakata na mapanga kisha kukimbia kusikojulikana
hadi alipogundulika
amejinyonga.“ Alielezea Kamanda Edmundi Urio.
Bw.
Urio alieleza kwamba Marehemu alikuwa na ugomvi na mke wake kwa muda
mrefu kitu
kilichopelekea mwanamke huyo kutoroka nyumbani kwake na kukimbilia
kwenda kuishi
Tanga inakodaiwa kuwa ni kwa baba yake mzazi.
Kamanda Edmund Urio alisema,
baaada ya kukaa muda mrefu bila kumuona mke wake marehemu alikuwa na
wasiwasi
kuwa ameolewa, hivyo aliamua kumtafuta mke wake huyo na ndipo alipoamua
kwenda
kwa mtendaji wa Kijiji hicho cha Kikombo Bw. Wenos Dede kuomba barua ya
kumtafuta mke wake Tanga na kupatiwa barua hiyo.
Aidh Bw. Urio alieleza
kwamba Jana majira ya saa mbili usiku marehemu na mke wake wakiwa
wanarudi toka
Tanga walipewa maelekezo kwamba, wafike kwanza kwa mtendaji kumjulisha
na kwa
usuluhishi zaidi, walipofika hawakumkuta
mtendaji kwa kuwa alikuwa
amekwenda kuhudhuria semina ya mambo ya
Sensa katika Kijiji cha Ihumwa.
“Hivyo wakiwa njiani
walishindwa kuelewana, kwani mwanamke alikuwa anataka kwenda kulala kwa
bibi
yake hapo hapo kijijini, ili kesho yake wamtafute mtendaji ili
wamalizane
lakini mume wake alikataa na kumwambia amsubiri akachukue shuka ndipo
akakimbia
nyumbani kwao akachukua Hengo na kulificha katika koti kisha kurudi na
kuanza
kumshambulia mke wake.” alieleza Kamanda Urio.
Kaimu Kamanda huyo
wa Mkoa wa Dodoma, alimtaja mwanamke huyo aliyejeruhiwa kuwa nia Aksa
John,
mwenye umri wa miaka (21), mgogo na mkazi wa Kikombo, pamoja na mtoto
wake
aitwaye Gerald John mwenye umri wa miaka (4) aliyejeruhiwa kwa kukatwa
Panga
katika mguu wake wa kushoto.
Alisema
mwanamke
huyo amejeruhiwa kwa kukatwa na panga mkono wa kulia chini ya kiganja,
na mkono
wa kushoto kidole chake gumba kilikatwa kabisa pamoja na kujeruhiwa
katika mguu
wa kushoto karibu na sehemu ya kukanyagia.
