SENSA YA MWAKA HUU YATAJWA KUWA KIPIMO KIZURI CHA MAENDELEO

 
SENSA ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika kote nchini Agosti 26 mwaka huu,imetajwa kuwa kipimio muhimu kwa hatua ya maendeleo yaliyofikiwa na wilaya ya Bunda mkoani Mara tangu ilipotangazwa kuwa miongoni mwa wilaya masikini zaidi nchini.

 Kwa mujibu wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP katika taarifa zake za mwaka 2002 ziitaja wilaya ya Bunda kuwa miongoni mwa wilaya masikini zaidi nchini.
 
Taarifa hiyo ya UNDP imetaja wilaya ya Bunda imekuwa ya mwisho kwa umasikini kutokana na kutokuwepo kwa upatikanaji wa uhakika wa huduma muhimu za kijamii kama maji,barabara,miundombinu na afya pamoja na uwepo wa makazi duni miongoni mwa wakazi wake.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Bw Joshua Mirumbe,ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa makarani watakaoshiriki katika zoezi la sense wilayani humo, ambapo amesema lengo kuu la sensa ni kupata taarifa mbalimbali za kimaendeleo zikiwemo takwimu za idadi ya watu na makazi jambo ambalo sasa kupitia taarifa hizo kutawezesha kuona kama Bunda ama imepiga hatua au inazidi kudumaa kimaendeleo.

Hivyo Bw Mirumbe ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kwa umoja na mshikamano kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi hilo kwa kuwapa ushirikiano makarani taarifa sahihi zitakazosaidia kuionesha wilaya hiyo mahala ilipo kimaendeleo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo