MUSOMA
BARAZA
la
madiwani limeikataa kupokea taarifa za upokeaji na ugawaji wa vocha za
ruzuku
za pembejeo za kilimo zenye thamani ya zaidi ya milioni 370 baada ya
kubaini kuwa
hakuna pembejeo ambazo zimewahi kufikishwa kwa wakulima wa halmashauri
hiyo
katika msimu wa kilimo wa mwaka 2011/2012.
Uamuzi
huyo
umefikiwa katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani chini
mwenyekiti wake
Bw Magina Magesa,ambapo kwa pamoja madiwani hao baada ya kukataa
taarifa
hiyo wameunda tume ya watu sita ili kuchunguza tuhuma hizo.
Wakizungumza
kabla ya kuundwa kwa tume hiyo,baadhi ya madiwani hao bila kujali
itikadi za
vyama vyao,wamedai kuwa hakuna hata kijiji kimoja cha halmashauri hiyo
kilichowahi kupokea pembejeo hizo za kilimo kama taarifa hiyo
ilivyonyesha huku
ikitaja kuwa ununuzi wa pembejeo hizo umeigharimu serikali kiasi hicho
cha
fedha.
Akizungumza
katika
kikao hicho,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw Magina Magesa,amesema
kitendo
ambacho kimefanywa na idara ya kilimo katika kitengo cha vocha za ruzuku
za
pembejeo,licha ya kuwa ni cha hujuma kubwa kwa wakulima,maendeleo ya
halmashauri hiyo pia kitafanya wananchi kukichukia chama cha mapinduzi
na
serikali yake endapo hatua za kisheria hazitachukuliwa dhidi ya wahusika
baada
tume hiyo kuwasilisha taarifa yake.
Hivi
karibuni
mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tupa,alibaini baadhi ya halmashauri katika
mkoa wa
Mara kutumia vibaya vocha za pembejeo za ruzuku zingine zikiuzwa nje ya
nchi
huku wakitumia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kusaini katika
vitabu
maalum vya kupokelea vocha hizo kwa kuwafanya ni wakulima ambao
walistahili
mgao huo.
