MWANAMKE
mmoja
mkazi wa Kilototoni wilayani Moshi Vijiji amekutwa ameuwawa na watu
wasio julikana nje ya nyumba yake aliyo kuwa akiishi na kumjeruhi vibaya
kichwani.
Kaimu
kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro Koka Moita, alithibitisha kutokea kwa
tukio
hilo ambapo alisema majira ya saa 01:35 usiku Agusti 16 mwaka huu katika
eneo
la Kilototoni Wilayani Moshi Vijijini kulitolewa taarifa katika kituo
cha
Polisi Himo kwamba kunamfanya biashara moja amekutwa ameuwaa nje ya
Nyumba
yake.
Alisema
baada ya
askari kupokea taarifa hizo walikwenda hadi eneo la tuko na kuukuta
mwili wa
marehemu Monica John (59) ukiwa pembeni kidogo na nyumba yake na kwamba
uchunguzi waawali unaonyesha kuwa marehemu huyo ameuwawa kwa kipigo
kikali kutokana na kukutwa na majeraha sehemu za kichwani.
Kufuati
tukio
hilo la mauaji jeshi la polisi mkoani humo limetoa wito kwa wananchi
kuwa
makini na watu wasio wafahamu katika maeneo yao na kwamba endepo
watabaini
kuwepo kwa hali tofauti watoe taarifa polisi kwaajili ya ulinzi zaidi.
Moita
alisema
matukio ya mauaji yamekuwa yakitokea mara kwa mara kutokana na uzembe wa
wananchi kuto kutoa taarifa polisi mara wabainipo kuwa na hali isiyo
kuwa ya
kawaida katika maeneo yao
Aidha
ajeshi la
polisi mkoani hapa limemshikilia mume wa marehemu kwa mahoojiana zaidi
kuhusiana na tukio hilo la mauaji na kwamba mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hosptali ya mkoa ya Mawenzi kwa uchunguzi zaidi.
