Kiongozi wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven
Ulimboka, akiwa amebeba maua, na kuzungukwa na Madaktari wenzake na
wananchi wa kawaida waliofika kumlaki, mara alipowasili mapema leo
Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu nchini Afrika Kusini. Dk
Ulimboka alisema kuwa yuko fiti na anaweza kufanya shughuli zozote
atakazopewa kuanzia sasa.
Picha na jiachie blog