MKUU wa Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa
Gerald Guninita amewaomba wasimamizi na makarani wa zoezi la sensa
Wilayani
humo kutolihujumu zoezi hilo badala yake wafanye kazi kwa bidii na
uaminifu
mkubwa.
Guninita amelazimika kuwasihi wasimamizi
na makarani hao ambao asilimia 90 ni walimu wa shule za msingi na
Sekondari
kufuatia kuwepo kwa minong’ono kwamba fedha watakazolipwa ni kidogo
ikilinganishwa na matarajio waliyokuwa nayo hapo awali.
Akifungua mafunzo kwa makarani na
wasimamizi hao wa zensa, Guninita alisema Serikali wilayani humo
imewateua
watumishi wengi wa umma kufanya zoezi hilo kutokana na uvumilivu wao
wakati
yanapotokea matatizo ya kifedha hivyo, kuwasihi wawe wavumilivu ili
matokeo ya
kazi yao yaliletee taifa mafganikio.
“Nawashukuru sana walimu wa Kilolo ambao
hawakuonyesha mgomo wakati wenzao wapo kwenye mgomo, uvumilivu wenu
ndiop
umetufanya tuwaamini na kuwaingiza kwenye zoezi hili muhimu kwa
maendeleo ya
kitaifa, fedha zeni zipo na ninachowaomba muwe wavumilivu na mfanye kazi
kwa
bidii,” alisema Guninita.
Alisema matokeo ya kazi yao yatapimwa
baada ya kumalizika kwa zoezi hilo, hivyo ni wajibu wao kufanya kazi
kwa
kufuata kiapo watakachopatiwa kabla ya kulianza zoezi hilo ambalo
linatarajia
kufanyika wiki mbili zijazo.
Alisema
serikali inapenda kuona kuwa sensa ya watu na makazi ya mwaka huu
inapata
mfanikio makubwa ili kuwezesha kupata takwimu muhimu zitakazotumika
katika
kufanya maamuzi sahihi na kupanga mipango endelevu.
“Serikali
inaamini kuwa mtatumia juhudi na maarifa katika kufanikisha zoezi la
sensa, kwahiyo
ifanyeni kazi hii kwa uaminifu kwa kuzingatia viapo
watakavyopewa,”Guninita
alisema.
Awali
wakizungumza na mwananchi, sharti la kutotaja majina yao baadhi ya
makarani
walisema matarajio yao ya awali wakati wakiomba kazi hiyo yamekufa baada
ya
kuwa watakuwa wakilipwa sh 35,000 kwa siku badala y ash 65,000 ambayo
walikuwa
wamedokezwa.
"Mtumaini
yetu yamefifia kwa sababu kiasi hicho cha fedha tutakachokuwa tukilipwa
kila
siku ndicho kitakachowawezesha pia kugharamia mahitaji yatu mengine
ikiwemo
malazi kwa wale watakaokuwa mbali na maeneo wanayoishi na chakula, mara
ya
kwanza tulifikiri tunghelipwa sh 65,000," alisema mmoja wa makarani hao.
Pamoja
na kulalamikia malipo hayo, makarani na wasimamizi walioanza mafunzo yao
Agosti
9, walilalamika kuchelewa kulipwa fedha hizo kwa zaidi ya siku tatu.
Akiwahakikishia
kulipwa fedha zao zote, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kilolo.Mohamed
Gwalima alikiri fedha kwa ajili ya wasimamizi na makarani wanaoshiriki
mafunzo
hayo kuchelewa.
“Zimechelewa kwa sababu ya mfumo mpya wa fedha wa EPICOR. Lakini tumeshajulishwa za kuwalipa kwa siku tano za mafunzo yenu ziko tayari na nadhani mtalipwa msiwe na shaka, ” alisema.
Alibainisha
kuwa mfumo wa EPICOR ambao umeanza kutumika hivi karibuni unalenga
kudhibiti
matumizi hewa au yaliyo nje ya bajeti.