Mwenyekiti wa kamati ya sensa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro
Mjumbe wa kamati ya sensa wilaya na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu
Washiriki wakisikiliza kwa makini
Viongozi wa dini, walemavu na wamiliki wa nyumba za kulala
wageni wilayani Makete wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha
zoezi la sensa ya watu na makazi wilayani humo
Hayo yamebainika wakati kamati ya sensa wilaya ya Makete
chini ya mwenyekiti wake ilipokutana na makundi hayo kwa lengo la kuwapatia
elimu ya sensa ili nao wakapeleke elimu hiyo kwa jamii
Akiungumza na makundi hayo mjumbe wa kamati ya sensa ambaye
pia ni katibu wa CCM wilaya ya Makete Bw. Miraji Mtaturu amesema viongozi wa
dini wao wana nafasi kubwa ya kuonana na waumini wao hivyo amewaomba kufikisha
elimu hiyo kwa waumini wao
“unajua ndugu zangu viongozi wa dini ni kundi linaloaminika
kwa jamii, tunawaombeni elimu hii tuliyowapa mkaifikishe kwa jamii, maana
serikali inafanya kazi na kila mtu ikiwemo ninyi, siku zimebaki chache naomba
tusaidiane tafadhali”alisema Mtaturu
Amesema sensa ya watu na makazi itaisaidia serikali kutambua
idadi ya watu nchini pamoja na mambo mengine ambayo yatasaidia serikali
kuboresha huduma zake na maendeleo katika sekta mbalimbali hapa nchini
Kwa upande wake Bw. Edwin Moshi ambaye naye ni mjumbe wa
kamati ya sensa wilaya ameelezea umuhimu wa wakuu wa kaya kutoa taarifa sahihi
kwa makarani wa sensa na si kutoa taarifa za kubuni pamoja na kuhakikisha kila
mtu aliyelala kwenye kaya yake ahesabiwa
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa kila mtu kuhesabiwa mara moja
tu wakiwemo watoto wachanga na walemavu kwani wengi wao wamekuwa wakisahaulika
kuhesabiwa kutokana na dhana potofu iliyopo kwa jamii kuwa hawahusiki, na
kuongeza kuwa taarifa zitakazokusanya zitakuwa za siri na zitatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa
Amewatoa hofu wananchi kuwa taarifa hizo zitatumika kwa
ajili ya freemasons, kujua utajiri wa watu ili wafilisiwe pamoja na kuwahamisha
wananchi kwenye maeneo yao ,
hivyo wnanchi wasiwe na hofu, taarifa hizo zitatumika kwa ajili ya maendeleo ya
nchi
Akihitimisha mwenyekiti wa kamati ya sensa wilaya ambaye pia
ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amewaambia waalikwa hao kuwa
wao ni wadau wazuri katika kufanikisha zoezi la sensa wilayani humo huku
akiwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni kutoa elimu kwa wahudumu wao na
kutambua kuwa usiku wa kuamkia Agosti 26 wawaambie wageni wao kuwa wajiandae
kuhesabiwa usiku huo
Ameongeza kwamba Agosti 25 kuamkia Agosti 26 sensa
itafanyika katika makundi tete ikiwemo kwenye nyumba za kulala wageni kwa kuwa
wageni hao wengi wao asubuhi hawapatikani, na makarani watakaotekeleza` zoezi
hilo watakuwa na vitambulisho maalum
Zoezi la uhamasishaji wananchi kushiriki sensa ya watu na
Makete usiku wa kuamkia Agosti 26 linaendelea wilayani Makete ambapo tayari
uhamasishaji umefanyika hii leo katika kata za Tandala, Iwawa, Bulongwa na
Matamba zoezi linaloongozwa na kamati ya sensa wilaya ya Makete na linaendelea
wilaya nzima


