MERERANI YARUDISHIWA VYANZO VYAKE VYA MAPATO NA SIMANJIRO

SIMANJIRO.
 
Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara imerudishiwa vyanzo vyake vya mapato ambavyo awali vilikuwa
vinakusanywa na Halmashauri ya wilaya  ya Simanjro.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Albert Siloli wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alibainisha kuwa  kuanzia mwezi huu wa Agosti halmashauri ya wilaya hiyo itawawekea kwenye akaunti yao fedha walizozikusanya mwezi huu katika eneo hilo .

Aidha alisema kuwa  baada ya kuzungumza na kukaa mezani kwa muda mrefu hatimaye viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo wamewarudishia vyanzo vyao vya mapato walivyokuwa wanavikusanya kwenye mji huo wa Mirerani.

Pia alivitaja vyanzo hivyo vya mapato kuwa  ni pamoja na machinjio,kituo cha magari ya abiria,soko na mnada wa Songambele na ushuru kwa watu
wanaolala kwenye nyumba za wageni katika mji huo.

“Kwa dhati ya moyo wangu naushukuru uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro wakiongozwa na Mkurugenzi wake Alhaji Muhammad Nkya kwa kuturejeshea vyanzo vyetu vya mapato,” alisisitiza Siloli.
 
Alieleza kuwa kwa muda mrefu wajumbe wa mamlaka ya mji huo walikuwa wanalalamikia kitendo cha halmashauri ya wilaya hiyo kukusanya ushuru na kuchukua mapato kutoka kwenye mji huo kisha wanawarejeshea kiasi kidogo cha mapato yao .
 
Alisema kuwa wapo  katika mchakato wa kuwafahamisha watu wote waliokuwa na tenda ya kukusanya mapato na kuyapeleka wilayani ili watambue kuwa fedha zetu zinabaki hapa hapa kwenye mji wetu wa Mirerani..

Vile vile wakazi wa mji huo bado wanasikitishwa na kitendo cha makampuni makubwa yanayochimba madini ya Tanzanite kutokuchangia
chochote kwenye mji huo huku wenye meza za pool table wakitozwa ushuru wa sh200 kila siku.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo