BABATI
KAMATI
ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Manyara imefanya ukaguzi kwenye barabara ya lami iliyotengenezwa kutoka Minjingu,Babati,Dareda hadi Katesh ambayo inadaiwa kuanza kuharibika kabla haijakabidhiwa kwa Serikali.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa huo,Elaston Mbwilo wakati alipotembelea barabar ambapo alibainisha kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kuelezwa na wananchi kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 223 imeanza kuharibika na hivi sasa inakarabatiwa.
Alieleza kuwa kuwa yeye na kamati yake wamefanya ukaguzi huo katika
barabara hiyo ambayo imegharimu kiasi cha zaidi ya sh200 bilioni na
inatarajiwa kukabidhiwa Serikalini wakati wowote kwenye mwezi huu wa
Agosti.
“Rais Jakaya Kikwete alishatuagiza kuwa kila mahali kwenye miradi
mikubwa inatakiwa tuwe tunafuatilia kama kuna matatizo lolote hivyo
mimi siwezi kukaa ofisini huku mambo yana haribika lazima nifuatilie,”
alisisitiza mkuu wa mkoa huyo.

Pia
yeye kama kiongozi
hawezi kusikia uharibifu unatokea na kukaa
kimya mpaka watu kutoka Dar-es-salaam,Singida au Dodoma waje
kulalamika lazima ashuhudie na kubaini na pia tatizo lipatiwe
ufumbuzi.
kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara wa
mkoa wa Manyara Tanroads Yohane Kasaini aliongeza kuwa ukarabati unaofanyika kwenye barabara hiyo unatokana na uharibifu uliofanywa na mvua zilizonyesha.
Alisema kuwa kitaalamu mvua zinaponyesha na kuingia barabarani lazima zilete madhara na pia barabara ya lami huwa hazipatani na maji hivyo pindi yakiingia tu lazima yalete madhara na ndipo uharibifu hutokea.
Naye Mhandisi msimamizi wa barabara hiyo,Godfrey Kombe
alisfafanua kuwa barabara hiyo hata ikikabidhiwa kwa Serikali inaendelea kuwa kwenye uangalizi wa kampuni zilizojenga kwa muda wa mwaka mmoja.
Alisema kuwa hata kama barabara hii itakabidhiwa kwa Serikali kampuni zote mbili zilizojenga zitakuwa zinawajibika kwa uharibifu wowote utakaotokea kwenye barabara hii ya Minjingu hadi Katesh.
Kuanzia Minjingu hadi Dareda wilayani Babati barabara hiyo
imetengenezwa na kampuni ya China ya Chico na kuanzia Dareda hadi
Katesh wilayani Hanang’ barabara hiyo inajengwa na kampuni ya China ya
Syno Hydro.