Korogwe
MBUNGE wa jimbo la Korogwe vijijini CCM Stephen Ngonyani amesema kwamba kamwe kwa muda huu hatarajii kujihusisha na malumbano na vyama vya siasa badala yake kazi aliyonayo ni kuendelea kuskiliza kero za wapiga kura wake ili kutafuta njia ya kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuendelea na utaratibu wake wa kutekeleza hadi zake alizowaahidi kwa njia ya vitendo.
Ngonyani almaarufu maji marefu alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa kwenye tarafa ya Bungu ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara huku akiwa ameambtana na mbunge wa Mtera CCM Livingston Lusinde na yule wa jimbo la Donge Zanzibar Sadifa Juma kama sehemu ya kutoa shukrani zake kwa wananchi mara baada ya kumpa kura za ubunge.
Alisema kwamba kitu ambacho anakihisi ni deni kubwa kwa wananchi wake ni kutekeleza ahadi zake jambo ambalo ameanza kulifanya hivi sasa kila anapopata fursa ya kufanya hivyo ambapo pia shughuli yake nyingine ni kusikiliza kero za wananchi ili kuweza kutafuta njia ambayo itasaidia kuzipatia ufumbuzi na kuwawezesha kupiga hatua za maendeleo kiuchumi.
"Labda ni waambie wananchi,mimi kwa sasa naomba mnielewe kwamba...na huu ni ujumbe kwa wale wanaonichafua kwa chuki binafsi,sina muda wa kujihusisha na malumbano ya vyama vya siasa wala mtu mwenye chuki nami za kisisa ila ninachofanya ni kutekeleza ahadi zangu nilizowaahidi na kusikiliza kero za wananchi,naombeni mnitumie"alisema maji marefu.
Katika mkutano huo mbunge huyo wa jimbo la Korogwe vijijini alipata fursa ya kuwaeleza wananchi mambo ambayo aliyaahidi na tayari ameyafanyia kazi na huku mengine akiendelea kuyafanyia kazi ambapo pia litoa misaada mbalimbali ya fedha taslimu kama sehemu ya mkakati wake wa kuhakikisha kwamba wapiga kura wake kero zilizowakabili awali zinaweza kutatuliwa.
Akiwa eneo la Mombo mbunge huyo aliweza kuwasaidia ulpaji wa ada ya leseni za lena na GRR vijana waendesha bodaboda zaidi ya 200 ambapo alitumia kiasi cha Tsh 2.7 ikiwa ni fedha taslimu kama sehemu ya kutekeleza ahadi zake ambapo kwenye katika eneo la Mkomazi alikipatia kikundi cha vijana mashine ya kuendesha kilimo cha umwagiliaji wa bustani za mbogamboga.
Mbali na kutoa misaada hiyo ambapo alikuwa akitumia fedha zake za mfukoni licha ya zile za mfuko wa jimbo mbunge huyo aliwataka wananchi waelewe kwamba wapinzania na wale wote wanaopita kaeneo mbalimbali wakimchafua hawana lengo la kuwatakia mafanikio akiwasihi kuwapuuza na kumpatia ushirikiano ili aweze kuwatumikia kikamilifu wananchi walio wengi.
Kwa upande wake Livingstone Lusinde ambaye ni mbunge wa Mtera CCM na mjumbe wa NEC aliwataka wananchi wa jimbo la Korogwe kumuenzi mbunge wao huyo ambaye alimueleza kuwa mwenye mapenzi makubwa na watu wake ambaye wakati wote ameonyesha ari ya kujitolea akiwa na lengo la kuwaharakishia maendeleo kwa kuwatatulia kero mbalimbali katika maisha yao.
"Mimi niwaambieni wanaKorogwe,hii ni tunu mmepata,mkiichezea hii mtakuja kulia,hebu niambeni wenyewe ni mbunge gani ambaye aliwahi kufanya kama haya anayofanya maji marefu katika uongozi wake?,wanapita hawa wanasema eti aende kwao,wale wanasema CCM haijafanya kitu au hajafanya kitu hebu waulizeni wao wamefanya nini,msimuache maji marefu"alisema Lusinde akiwataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaoimchafua mbunge huyo akiwaita waroho wa madaraka.
Mbunge huyo wa jimbo la Mtera aliwabainishia wananchi kuwa hivi sasa kuna utitiri wa vyama ambavyo vina sifa na uwezo mkubwa wa kuorohesha kero za wananchi huku wakishindwa kuzitatua nkama ilivyo kwa CCM hivyo amewaasa wananchi kuwa macho na kuwapuuza wanasisa uchwara ambao hawana nia njema na wananchi ambap wengi wao wana hali duni za maisha.
Vilevile Lusinde katika mkutano huo aliwasihi wananchi ambao ni wanaCCM kuepuka kuwachagua wala rushwa kwenye nafasi za wajumbe wa NEC akisema kwamba iwapo itabainika wamewapa fursa watu wa aina hiyo basi wajue dhahiri kwamba majina hayo yatakatwa kwa kuwa yeye binafsi akiwa mjumbe atashinikiza ifanyike hivyo akiwasisitiza kuwachagua watu wenye uwezo.
Naye mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo alipopata fursa ya kuwasalimia wananchi kama sehemu ya kujitambulisha kwao tangu ateuliwe rasmi kushika wadhfa huo katika wilaya hiyo,aliwataka kumpatia ushirikiano katika kutambua kero zote zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kumpatia taarifa za wale wanaohujumu serikali ya chama tawala ili awashughulikie kisheria.