Kagera
Halmashauri
ya wilaya ya Chato Mkoani Kagera inakusudia kubinafsisha mpango wa
ujenzi wa
nyumba za walimu baada ya majadiliano yanayoendelea baina yake na
serikali za
vijiji ili kupata ardhi kwa ajili ya mpango huo.
Hatua
hiyo inalenga kukabiliana na tatizo la uhaba mkubwa wa nyumba za walimu
ambalo
wadau wanalielezea kuwa miongoni mwa sababu za kudorora kwa maendeleo
ya
elimu wilayani humo.
Katika
ripoti ya utafiti wa Mradi wa Uwezo Tanzania 2011, wilaya ya Chato
ilishika
nafasi ya 66 miongoni mwa wilaya 132 zilizofanyiwa utafiti nchini katika
stadi
za kusoma Kiswahili, Kiingereza na kufanya Hisabati za kiwango cha
darasa la
pili.
Kwa
mujibu wa viongozi wa halmashauri, wilaya ya chato ilikuwa na upungufu
wa
nyumba 1615 za walimu ambao ni sawa na aslimia 87.5 ya mahitaji ya
nyumba 1845
kwa ajili ya kuwawezesha walimu kuishi kwenye mazingira ya shule zao.
Ofisa
elimu wa Wilaya ya Chato Ishengoma Kyaruzi alisema uhaba wa nyumba za
walimu ni
miongoni mwa maeneo ya vipaumbele vya halmashauri hiyo ambayo yanakwazwa
na
ukosefu wa raslimali ikiwamo fedha na ardhi.
Alisema
kuwa mbali na kutafuta ardhi, halmashauri ya wilaya hiyo ilikuwa
inaandaa
utaratibu wa kuwapata wawekezaji ambao watajenga nyumba na baadaye
kuzipangisha
kwa walimu kwa malipo nafuu.
Alidokeza
mkakati huo wakati akitoa mada kwenye mdahalo ulionadaliwa na Asasi za
Kiraia
Mkoani Kagera kwa ubia na The Foundation for Civil Society kujadili
changamoto
za elimu.
Naye
katibu wa Chama Cha Walimu wilayani Chato Victoria Laurent alisema kuwa
kukosekana kwa nyumba za walimu kwenye maeneo ya shule kumeathiri
viwango vya
taaluma kwa kiasi kikubwa.
“Tunaomba mamlaka kujenga mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia
ambayo
bila kuwapo ndoto zakufikia malengo ya millennia zitakuwa zimeishia
hewani”
alisema Kiongozi huyo wa CWT.
Alisema
kutokana na walimu kuishi mbali na shule ilikuwa vigumu kuwahi ratiba za
masomo
sambamba na kushindwa kuzuia uharibifu wa mali na samani za shule
unaotokea
baada ya saa za masomo.