Tarime.
MAMLAKA ya Mji Mdogo wa Tarime
kupitia vyanzo
vyake vya ndani vya mapato imekusanya jumla ya 220,788,095.97 sawa na
asilimia
85% ya kiasi kilichokuwa kimekasimiwa kipindi cha mwaka wa fedha
ulioishia
tarehe 30 mwezi juni 2012.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa
mamlaka ya
mji mdogo wa Tarime Christoper Mantago wakati wa kikao cha wajumbe wa
baraza la
mamlaka ya mji huo,Mantago alisema kuwa kwa kipindi hicho mamlaka ya
mji
ilikisia kutumia jumla ya 260,026,600 na kiasi halisi kilichotumika ni
212,811,995.95
sawa na asilimia 82 ya matumizi yaliyokasimiwa.
Pia Mantago alisema kuwa katika
upande wa
usafi wa mazingira mamlaka hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya sita
Kitaifa na
kwamba malengo yao ni kushika nafasi ya kwanza.
Mantago alisema kuwa pamoja na
juhudi hizo
za mamlaka katika makusanyo bado mamlaka hiyo inakabiliwa na tatizo la
kutokuwa
na baadhi ya wataalamu wanaohitajika hususani mwanasheria na muhandisi
wa
ujenzi.
Aliongeza kuwa baadhi ya wafanya
biashara
wanaotumia vibanda vilivyoko soko kuu na stendi ya mabasi kwa
kutokuafikiwa
kusaini mkataba utakao wawezesha kulipa mamlaka ya mji kodi ya vibanda.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime John
Henjewele
aliipongeza mamlaka hiyo kwa makusanyo mazuri ya mapato kupitia vyanzo
vyake
vya ndani ambapo aliwataka kuzidi kuongeza zaidi makusanyo huku
akisisitiza
siasa isihusishwe katika maendeleo ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa
Tarime
kwani inakwamisha maendeleo.

