Tarime.
MAMLAKA ya Mji mdogo Tarime imeunda
kamati
ndogo kwa ajili ya kuchunguza eneo la wazi la Serikali lililoko
kitongoji cha Mwangaza kata ya Nyamisangura Wilayani Tarime uliodaiwa
kuuzwa na
wataalamu wa mipango miji na ardhi wa mamlaka ya mji mdogo kwa kanisa
la EAGT Tarime.
Uamuzi huo wa kuundwa kwa kamati
ndogo umekuja
baada ya kudaiwa kuwa kuna uwanja wa wazi uliotengwa na Serikali kwa
ajili ya kujengwa Zahanati na shule ya awali lakini matokeo yake
wataalamu wa
ardhi wa mipango miji wameuza eneo hilo la wazi kwa kanisa la EAGT.
Wajumbe wa Baraza la mamlaka hiyo
walisema kuwa
wameshangazwa kwa kitendo cha wataalamu kuuza eneo la Serikali kwa
kanisa
huku wakijua eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya Shule na Clinic.
Ofisa mipango miji wa mamlaka ya mji
mdogo
Tarime Nzengula Wilfred alisema kuwa eneo hilo la EAGT taratibu zote
zilifuatwa kutoka kwa kamishna wa Ardhi na kwamba tatizo la ufahamu
mdogo
wa wajumbe kuhusu maswala ya ardhi ndiyo chanzo cha kuibua migogoro.
Hata hivyo maelezo ya Ofisa mipango
miji
yaliwakwaza wajumbe ambapo walimtaka ofisa huyo kufuta kauli yake kwa
kile
alichodai kuwa wajumbe wana uwelewa mdogo kuhusu ardhi.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwangaza
Joseph
Maseke na wajumbe wengine wakaomba watafutwe watu waliolipwa fidia na
Serikali mwaka 1998 ili kuthibitisha kwakuwa wapo hai kutokana na madai
ya kanisa la EAGT kudai kuwa wao ndio waliolipa fidia wananchi.
Hali hiyo ya wajumbe wote kuwalalamikia
wataalamu kwa kuuza eneo la Serikali na kuomba iundwe kamati ndogo ya
uchunguzi
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Tarime Christopher Mantago alichagua
kamati
ndogo ya wajumbe 6 watakaofanya uchunguzi kati yao 3 wanaotokea eneo la
Ronsoti
na mwangaza kuliko na kanisa la EAGT,wajumbe wawili kutoka mamlaka ya
mji mdogo
na mmoja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.