MABASI YANAYOTUMIA STENDI YA MOSHI MJINI YATAKIWA KULIPA USHURU MPYA

Moshi

MKURUGENZI wa manispaa ya moshi mkoani Kilimanjaro, Bernadette Kinabo
  amewataka madereva wanaoingiza magari yao katika stendi kuu ya mabasi moshi kulipa ushuru ulioongezeka na kuacha kulumbana kwa kuwa kiwango kilichoongezwa hakita badilishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusiana na

madereva wanaoingiza magari katika stendi na kukataa kulipa ushuru kwa madai kuwa ushuru huo umeongezwa bila kushirikisha madereva hao, Kinabo alisema kiwango hicho hakitabadilishwa na wanatakiwa kulipa ili manispaa iweze kujenga barabara zote kwa kiwango cha lami.

Kinabo alisema madereva hao wanakataa kulipa kutokana na wakala

aliyepewa tenda ya kukusanya ushuru ndani ya manispaa hiyo kushindwa
kusimamia zaezi la kupanga magari na kukusanya ushuru huo

“tumeongeza ushuru kutoka shilingi 500 hadi 1500 kwa mabasi madogo na
  shilingi 1000 hadi 2000 kwa mabasi makubwa yanayokwenda mikoani , kwa sababu tumekaa muda mrefu sana bila kuongeza ushuru takribani miaka kumi sasa”alisema kinabo.

Mkurugenzi huyo alisema zoezi hilo limekwama kutokana na wakala

aliyepewa tenda hiyo kushindwa kupanga magari  na kutoza ongezeko hilo na kwamba manispaa inaweka wakala mwingine ambaye ataweza kusimamia zoezi la kutoza vingo vya ushuru vilivyoongezeka.

Nao baadhi ya madereva hao ambao ni Daniel Kimwaga, Muhamed bonge na
  Mwidoe Rajabu  walisema hawatalipa kiwango hicho na badala yake
watalipa kiwango cha zamani ambacho walichokubalina na manispaa hiyo
kutokana na manispaa kutowashirikisha madereva hao kuhusiana na
mabadiliko ya ushuru  huo.

Walisema hawatolipa kwa sababu hakuna babadiliko yoyote yaliyofanywa

tangu waanze kulipa ushuru huo na kwamba mabasi mengine hayana sehemu ya kuegesha bali wanaegesha pembezoni mwa barabara.

Madereva hao walisema ni muda wa mwezi mmoja na nusu sasa tangu waache
  kulipa ushuru kutokana na manispaa kuongeza ushuru huo kupita kiasi na kutofanya mabadiliko yoyote katika stendi hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo