MOSHI
BARAZA kuu la waislamu (BAKWATA)mkoani Kilimanjaro limakana kuhusika juu ya vipeperushi vinavyosambazwa kushawishi watu wasishiriki katika sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika ushiku wa kuamkia augusti 26 mwaka huu.
Akizungumza katika kikao cha dharura cha baraza hilo,shekhe mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Sheikhe Shaban Rashid amesema wao kama baraza
hawahusiki na vipeperushi hivyo na kwa yeyote anayehusika yafaa
kuchukuliwa hatua kali.
Sheikhe Shaban ameyasema hayo baada ya kukamatwa kwa watu sita
wilayani mwanga na wilayani same ambapo amesema kitendo cha kusambaza vipeperushi hivyo kwa dini ya kiislamu ni aibu kwani ni kuipinga
serikali kwa kutotii maagizo yake ambayo ni kwa manufaa ya wananchi
wake na waislamu pia.
Ameongeza kuwa,kitendo hicho ni kupinga juhudi za serikali za
kuhakikisha wananchi wake wanapata maisha bora na kupata takwimu
kamili ili waweze kuwasaidia wananchi wote .
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo sheikhe Ramadhan Salim
amewataka waislamu mkoani hapa kuwapuuza wanaosambaza vipeperushi hivyo na kuunga mkono jitihada za serikali ili kufanikisha zoezi hilo ambalo ni kwa manufaa ya taifa zima na waislamu kwa ujumla sanjari na kuwaonya wale wanaotaka kugomea zoezi hilo kutokufanya hivyo kwani ni kinyume na taratibu za dini ya kiislamu.