JESHI LA POLISI MANYARA LAFANYA MSAKO KUIMARISHA DORIA


MANYARA.

Imebainishwa kuwa ili kupambana na uhalifu jeshi la polisi mkoani Manyara linafanya msako na kuimarisha doria katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa manyaya.
 
Hayo yamebainishwa na kamanda polisi mkoa wa Manyara Akili Mpwapwa wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa habari mkoani hapa.
 
Alibainisha kuwa  katika msako huo watuhumiwa wa makosa mbalimbali wamekamatwa kwakukuhusika na matukio ya uhalifu kama vile  kupatikana na kwa Bhangi,mirungi na makosa ya usalama barabarani pamoja na pombe aina ya moshi gongo.
 
Kamanda Mpwapwa alisema kuwa katika kupatikana  na silaha na risasi bila kibali katika barabara kuu itokayo Arusha Babati walikamatwa watuhumiwa wawili Salimu Mohamed na Paulo Issa wakiwa na bunduki moja aina ya rifle 458 no 59477,risasi sita,maganda mawili na risasi nyingine ndogo mbili  ambazo hazijafahamika ni za bunduki gain.
 
Aliendelea kusema kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa walikiri kuwa wao ni majangili na walikuwa safarini kwenda kuwinda Tembo katika hifadhi ya Tarangire kupitia Galapo,watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.
 
Alisema kuwa huko maeneo ya Mdori Hamisi Gidamrisi Giau alikamatwa na bunduki rifle 458 no 987660 ambayo nayo alikiri inatumika na ujangiri naye amefikishwa mahakamani.
 
‘’Jamani waandishi wa habari kiasi cha 27 kg za Baghi zilikamatwa sehemu mbalimbali za mkoani hapa pia katika msako huo watuhumiwa sita walikamatwa kwa makosa ya kupatikana  kwa Baghi na kiasi cha mirungi 160 kg zilikamatwa katika msako watuhumiwa watatu walikamatwa watuhumiwa  wote wamefikishwa mahakamani.’’Alisema Kamanda Mpwapwa.
 
Aliongeza kuwa  kutokana na msako uliofanywa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara kiasi cha lita 1713 za pombe haramu ya moshi(gongo) zilikamatwa,jumla ya watuhimiwa 82 walikamatwa na kufikishwa mahakamani,kati yao 62 walipatikana na  hatia,wengine 20 kesi zao zinaendelea na  mitambo sita ya kutengenezea gongo ilikamatwa katika misako hiyo.
 
Kamanda Mpwapwa alisema kuwa kwa upande wa udhibiti wa makosa ya uaslama Barabarani jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 519,makosa ya ubovu wa vyombo vya usafiri ni 85,makosa mengineyo ni 434 ambapo  jumla ya shilingi milioni 15,570,000 zilikusanywa kutokana na faini ya papo kwa hapo.
 
Alisisitiza kuwa  jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kwa zoezi zima la msako na kudhibiti makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha mwezi julai 2012 kutokana na mahusiano mazuri baina ya jeshi hilo na raia wema ambao wamewezesha kwa njia moja au nyingine kutoa taarifa zilizoleta mafanikio katika chombo chao cha jeshi hilo kwa kuzingatia sera ya jeshi la polisi Tanzania kuimarisha ulinzi shirikishi na polisi jamii.
 
Ametoa wito kwa wananchi wa mkoani hapa kuondoa wasiwasi na kutoa taarifa katika chombo chao cha jeshi la polisi ili kuweza kufanikisha kukamata na kuzuia au kupunguza uhalifu ndani ya mkoa huo na kwamba siri zao zinatunzwa.
 
Pia alimalizia kwa kuwaonya wananchi ambao wanaojihusisha na vitendo vya uharifu kama vile unyang’anyi wa kutumia nguvu,kupatikana na baghi,mirungi na makosa ya usalama barabarani kuacha vitendo hivyo mara moja ambapo jeshi hilo limejipanga vizuri kupambana na uhalifu wa aina yoyote wale wataendelea kujihusisha na vitendo vya uhalifu watakamatwa na kufikishwa mahakami ili sheria ichukue mkondo wake dhidi yao .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo