Rombo.
ZAIDI ya
Tembo tisa wamevamia kijiji cha Mahida Mangoni wilaya ya Rombo mkoani
Kilimanjaro,
na kuua mtu mmoja na kujeruhi pamoja na
kuharibu mazao ya migomba.
Mkuu wa
wilaya hiyo Elinasi Pallangyo alisema tembo hao waliigia kjijini hapo na
kuanza
uharibifu huo haliiliyopekea wananchi kuanza kuwafukuza na hatimae tembo
hao
kuua mtu mmoja pamoa ja kujeruhi.
Alisema baada
ya tembo hao kuua wananchi mmoja na kujeruhi, wananchi hao
waliwashambulia
tembo hao na kuua tembo mmoja.
Mkuu huyo
amewataka wananchi wilayani humo kutosumbua wanyama hao pindi
wanapoingia ndani
ya wilaya hiyo na badala yake kutoa taarifa kwa vituo vya askari vya wanyama pori vilivyopo wilayani humo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa
Robert Boaz
amethibitisha kutokea kwa kutukio hilo na kwamba lilitokea agusti 10
mwaka huu
majira ya saa 8:00 mchana na ambapo tembo hao walisababisha kifo cha
Veronica
John (44) na kumjeruhi vibaya Stiven Shirima.
Boaz alisema
marehemu alikuwa shambani akiwa anajishughulisha na shughuli za kilimo
ambapo
tembo hao walimkanyagakanyaga sehemu mbalimbali za mwili
pamoja na kuchumwa na pembe mbavuni upande wa
kushoto.
Kamanda huyo
alisema hali hiyo ilimfanya avuje damu
nyingi hali iliyopelekea kupoteza uhai na kwamba majeruhi wanapatiwa
matibabu katika
hospitali ya huruma huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhia katika
hospitali
hiyo.
