MUSOMA
MKOA wa Mara
umekamilisha tayari
umechukua hatua za haraka za kuhakikisha zoezi la Sensa ya watu na
makazi
linafanikiwa kama lilivyopangwa katika visiwa 30 ambavyo vimo ndani ya
ziwa
Victoria.
Mratibu wa Sensa
mkoa wa Mara Bw
Ramadhan Mbega,amesema mbali na kuyabainisha maeneo hayo pia imetenga
maeneo ya
kuhesabia watu katika maeneo ya hifadhi za taifa ya Serengeti na mapoli
ya
akiba yanayopakana na hifadhi hiyo.
Hata hivyo Bw
Mbega,amewataka
wananchi wa mkoa wa Mara kuachana na dhana potofu ya baadhi ya watu kuwa
endapo
watahesabiwa katika zoezi hilo wanaweza kupoteza maisha ama kushindwa
kuzaa.
Bw.Mbega amesema si
kweli kuwa watu
wanaweza kuzaa au kupoteza maisha na kuongeza kuwa zoezi hilo linalenga
kuwezesha taifa kupata takwimu sahihi za watu na makazi kwaajili ya
kuwahudumia
vema wananchi wake.
Mbali na hivyo
mratibu huyo
amempongeza mkuu wa mkoa wa Mara Bw.John Tuppa kwa kuwa mstari mbele
kuhamasisha wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa huku akitoa wito kwa
wananchi
kujitokeza katika zoezi hilo
Na www.mwanawaafrika.blogspot.com