BUTIAMA
Mahakama ya mwanzo
ya Kukirango katika wilaya ya Butiama mkoani Mara haina hakimu wa kudumu
na
hivyo kusababisha kesi nyingi kuahirishwa mara kwa mara.
Wakiongea katika
eneo la mahakama hiyo,baadhi ya wananchi wamesema kuwa kumekuwepo na
karani
mmoja katika mahakama hiyo ambaye kazi yake imekuwa kuahirisha kesi.
Wamesema kukosekana
kwa hakimu wa kudumu katika Mahakama hiyo baadhi ya kesi zimekuwa
zikiendeshwa
kwa zaidi ya miaka miwili, huku wengine wakipeleka kesi zao katika
Mahakama ya
mwanzo ya mjini Musoma.
Aidha wananchi hao
wamesema kuwa nyumba zilizojengwa wakati wa ukoloni kwa ajili ya hakimu
na
karani zimegeuka kuwa makazi ya popo na mchwa.
Mahakama ya Mwanzo
ya Kukirango inahudumia wananchi wa kata nne zilizopo katika tarafa ya
Makongoro ingawa kwasasa imeshindwa kutoa huduma ipasavyo kutokana na
kutokuwa
na hakimu wa kudumu.