Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Mekete kuwa
na desturi ya kufanya usafi wa mazingira wa maeneo yanayowazunguka kuanzia
ngazi ya kaya
Hayo yamezungumzwa na Afisa maendeleo ya jamii
wa kta ya isapulano bw, Denis Sinene wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira
katika kijiji cha luvulunge wilayani makete
Bw,Sinene amesema kuwa wapo wananchi wanaosubiri
hadi watangaziwe kuwa kuna ukaguzi wa usafi wa ndipo wanaanza kusafisha
mazingira yao
hali inayosababisha milipuko ya magonjwa mbalimbali miongoni mwa jamii
Aidha amesema kwasasa watafanya ukaguzi wa usafi
kimyakimya bila ya kutoa taarifa na pia kuwataka wakazi wa maeneo hayo kujenga vyoo vya kisasa
vya kutumia tofali nakuacha kutumia mabanzi katika kujenga vyoo hivyo
Na: Obeth
Ngajilo & Anitha Sanga