Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Ezekieli Maige katikati
Akiongea na waandishi wa habari leo .katika. Hafla ya kukabidhi ofisi
kwa waziri mpya wa wizara hiyo Mh Balozi Khamis Kagasheki ambaye ni wa
kwanza kushoto na Naibu Waziri wake Mhe.Lazaro Nyarandu ambaye ni
wa kwanza kulia.katika ukumbi wa mikutano wa wizara ya maliasili na
utalii jijini Dar es salaam.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Naibu Waziri wa maliasili na utalii Mhe. Lazaro Nyarandu akisisitiza
jambo katika hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi iliyofanyika leo katika
wizara ya maliasili na utalii.
Waziri wa maliasili na utalii Mh; Balozi Khamisi Kagasheki akiongea na
waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi leo ambapo
amesema watendaji wote walioguswa na kashfa mbalimbali katika wizara
hiyo watachukuliwa hatua za kisheria mara moja iwezekanavyo.
Aliyekuwa Waziri wa maliasili na utalii Mhe.Ezekieli Maige kulia
wakiingia ofisini na waziri mpya wa wizara hiyo na Naibu wake tayari kuanza kazi rasmi baada ya
kukabidhiwa ofisi leo.
Waziri wa maliasili na utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa wizara hiyo.
Waziri wa maliasili na utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki akiwa kwenye
picha ya pamoja na aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Mhe.Ezekieli
Maige mara baada ya makabidhiano ya ofisi leo.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria katika hafla hiyo
Picha kwa hisani ya fullshangwe blog


