Viongozi wa serikali za
vijiji wazazi na wadau wengine wa elimu wametakiwa kutoweka maslahi yao wenyewe katika
kuwanusuru wanafunzi kuondokana na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia mashuleni
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la
Support makete to self support (SUMASESU) Bw. Egnatio Mtawa wakati wa uzinduzi
wa mradi wa shule salama unaendeshwa na shirika hilo kwa ufadhili wa RFE
Amesema shirika la SUMASESU linajitahihidi
kuhakikisha jamii ya Makete inaishi kwa usawa, amani, maendeleo pamoja na kuwa
na afya nzuri na hilo
litafanikiwa
Mradi huo
wa shule salama utazihusisha shule nne za sekondari ya Itamba, Matamba,
Ikuwo na Mlondwe na mradi huu utaendelea
hadi mwezi wa Februari mwaka 2013
Na: Aldo
Sanga & Veronica Mtauka