Wananchi wilayani Makete wametakiwa kutoa
ushirikiano kwa kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi
inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti 26 mwaka huu
Hayo yamesemwa na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati
ya sensa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Zainabu Kwikwega wakati wa kikao cha wajumbe wa
kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete
Amesema pamoja na hayo pia anaipongeza hatua
iliyofikiwa na serikali kwa kufuta posho za vikao vya sensa nchi nzima kutokana
na uhaba wa fedha na kuwataka watu wote wanaotakiwa kufanikisha zoezi hilo
kufanya kazi zao kwa moyo na bila kinyongo ili zoezi hilo lifanikiwe
Katika kikao hicho wajumbe walijadili changamoto
mbalimbali zinazolikabili zoezi hilo
pamoja na namna ya kutatua changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha
wanahabari, viongozi wa dini, asasi zisizo za kiserikali pamoja na wadau
mbalimbali ili kufanikisha kufikisha elimu kwa jamii