Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Iwawa wilayani
Makete Bw. Fredy Chaula pamoja na walimu wa shule hiyo wamepongezwa kwa
ushirikiano walioutoa kwa maafisa maendeleo ya jamii wanaofanya mazoezi katika
kitengo hicho wakati walipofanya ziara katika shule hiyo
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja kati ya
maafisa hao Denis Sinene amewapongeza waalimu hao na kuwataka kuonesha ukarimu
huo hata kwa watu wengine watakaokuja kuhutaji ushirikiano wao katika kusukuma
gurudumu la maendeleo
Katika hatua nyingine maafisa hao wamewataka
wazazi na walezi wilayani Makete kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni,
kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamewasaidia waalimu kutatua changamoto za
elimu zinazowakabili wanafunzi na taaluma ya elimu itakuwa mwaka hadi mwaka
Amesema wazazi na walezi wakishirikiana pamoja
na waalimu watasaidia kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi ikiwemo
utoro shuleni hapo, kwani ni moja ya matatizo yaliyopo katika shule nyingi
Na Obeth Ngajilo
