Tanzania imetajwa kuwa miongoni
mwa nchi ambazo hazijaweza kutumia kikamilifu tafiti zake na hivyo kushindwa kufikia
malengo ya tafiti hizo
Wadau wa sekta ya teknohama sayansi na
teknolojia kutoka nchi 45 za Afrika na Ulaya wamekutana nchini humo kwa lengo
la kutafuta njia za kuwezesha nchi za bara la Afrika kuweza kufanya tafiti
mbalimbali na kuzitumia ili kuharakisha maendeleo ya nchi hizo
Hali hiyo hapa nchini inasababishwa na upungufu
wa rasilimali watu katika tafiti hizo kama
alivyosema Prof. Avelini Mbede Mkurugenzi kutoka tume ya mawasiliano na
Teknolojia
