NA
MWANDISHI WETU
KAMANDA
wa Kipolisi Mkoa wa Ilala Faustine Shilogile amesema suala la kupambana na dawa
za kulevya ni mtambuka hivyo ni wakati kwa kila mwanajamii kujitokeza katika
kupambana na tatizo hilo.
Kauli
hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akizungumza na
Fullshangweblog kuhusu kuibuka kwa vikundi vya vijana wanaojihusisha na
uvutaji
wa dawa hizo.
Alisema
wananchi wanapaswa kuondokana na mawazo kuwa mapambano ya udhibiti wa uingizwaji
wa mihadarati nchini yanalihusu
jeshi la polisi pekee bali mapambano hayo yanazihusu Wizara ya Kazi na Ajira,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Shilogile
alisema iwapo Wizara hizo, zitawajibika ipasavyo kwa kuyaunganisha makundi ya vijana
ambao wengi wao ndiyo waathirika wa kubwa wa matumizi ya dawa za kulevya katika
shrikisha katika miradi ikiwa ni pamoja kuwaanzishia mashindano mbalimbali ya
michezo.
“Unajua vijana wengi wa Tanzania wamekuwa
hawana ajira kutokutokana na hali hiyo hujikuta muda mwingi wakiwa hawana la
kufanya mwisho wasiku hujikuta wakitumiwa na baadhi ya matajiri kuwauzia dawa
hizo na hatimaye kuwa watumiaji hadi kuathirika na kupoteza uwezo wa kufanya
kazi hivyo kulifanya taifa kupoteza nguvu kazi”alisema Shilogile.
Shilogile
alisema wamekuwa wakijaribu mbinu mbalimbali hata kutumia michezo kwa lengo la
kuwashuhulisha vijana hao ili wasipate muda wa kuwaza mabo mbaya kama hayo.
Alitanabaisha
kuwa kuna mashindano ambayo ameanzishwa na Makanda na baadhi ya mikoa ikiwa ni
moja ya kampeni ya kuwaweka vijana katika mazingira kuondokana na msongo wa
mawazo wa ukosefu wa ajira ambao huwa unawasukuma katika kujiingiza kwenye
uhalifu.
Hata
hivyo, Shilogile alisema wamekuwa wakifanya opereshini mbalimbali za kuwakamata
wauzaji wa kati ambapo hadi sasa kuna baadhi wamekwisha wafungulia kesi
mahakamani.
Na fullshangwe blog