Nusu fainali ya pili kombe la Tunduma Cup 2012 ilikuwa kati
ya wauza simu wazee Bandari FC waliokuwa wakimenyana na na timu ya Mbinde's Fc mchezo uliomalizika kwa wazee wa bandari kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lawashindi limewekwa kimiani na mchezaji Charles Issa dakika ya kwanza na sekunde ya kwanza
kutokana na ushindi huo timu ya wazee wa bandari watacheza fainali na timu ya wauza dagaa maarufu kwa jina la small fish zote za Tunduma mkoani Mbeya
Fainali hiyo inatazamiwa kupigwa kati ya Jumamosi au Jumapili na itategemea na kamati ya mashindano itakavyokubaliana na mtanangehuo utapigwa katika dimba la shule ya msingi Tunduma
Na Keneth Ngelesi