MBUNGE MSIGWA AWEKWA KITIMOTO NA AZAKI ZA KIRAIA , YEYE ASEMA HATAWATETEA WAPIGA KURA WAKE WANAO JENGA KIHOLELA

MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amewataka wananchi wa jimbo hilo na watanzania kuendelea kupiga vita vitendo vya ufisadi kwa vitendo ikiwa na pamoja na wao wananchi kufanya kazi badala ya kuwanyoshea vidole mafisadi wakati na wao wananchi ni mafisadi wa muda.

Alisema kuwa kuvunjwa kwa baraza la mawaziri ni kutokana na wabunge kuchukizwa na vitendo vya ufisadi kwa mawaziri waliotemwa katika wizara zao na Rais Jakaya kikwete na kuwa hata baraza jipya lililoteuliwa sasa iwapo litaendeleza vitendo vya ufisadi kama lile lililovunjwa basi watashughulikiwa kama wenzao.

Mbunge Msigwa alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa chuo chamaendeleo ya jamii Ruaha katika mdahalo wa pamoja kati yake na wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini mdahalo ulioandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Iringa na kuratibiwa na asasi ya ICISO.

Alisema kuwa pamoja na jitihada mbali mbali zinazofanywa na wabunge katika kuchukizwa na vitendo vya ufisadi ila bado kwa upande wa wananchi pia wamekuwa wakishiriki kufanya ufisadi ambao ni mkubwa zaidi na wenye kulifanya Taifa kuendelea kuwa nyuma katika maendeleo kutoka na tabia ya baadhi ya wananchi kuendekeza uvuvi wa kushinda vijiweni bila kazi.

Hivyo alisema kuwa wakati mawaziri na viongozi wanatuhumiwa kwa ufisadi na kuondolewa katika nafasi zao bado wananchi nao wanapaswa kujitathimini kwa kufanya kazi kwa bidii badala ya kushinda vijiweni.

Aidha mbunge Msigwa alisema kuwa kamwe hatakuwa tayari kuwatetea wananchi wa jimbo lake ambao wanakiuka sheria za mipango miji kwa kujenga nyumba bila kufuata taratibu za mipango miji.

Kwani alisema kuwa kuendelea kuwatetea wananchi wanaojenga nyumba kiholela katika maeneo ya hifadhi ya barabara ni sawa na kujipalia makaa ya moto kwa madai kuwa leo ni serikali ya CCM ndio ipo madarakani ila ipo siku serikali ya Chadema itakuwepo madearakani hivyo kama wajunja sheria wataendelea kutetea nchi haitatawalika pia kwa Chadema.

Mbunge Msigwa asema kuwa yeye si mbunge wa kugawa samaki kwa wapiga kura bali ni mbunge wa kuwasaidia ndoano wapiga kura wake.

Hivyo lazima ataendelea kuwaongoza wapiga kura wake kufuata sheria na sio kuwatetea hata pale wanapokiuka ama kuendelea kuwahonga fedha kama njia ya ushawishi badala ya kuwapa mbinu za kuzifuata.

Aidha aliasema kuwa iwapo utaona mbunge anaendesha jimbo kwa fedha zake za mfukoni basi ujue ni mwizi ama ni mfanyabiashara mkubwa hivyo alisema kuwa hapendi kuwadanganya wapiga kura hao kuwa ataboresha miundo mbinu wakati serikali yenyewe imekwama kufanya hivyo

Mratibu wa midahalo hiyo Raphael Mtitu alisema kuwa mdahalo huo umeonyesha kufana zaidi na kuwa lengo la midahalo hiyo ni kuwakutanisha wapiga kura na wabunge wao ili kuongeza kasi ya maendeleo kwa matakwa ya wapiga kura.

Hata hivyo alisema midahalo kama hiyo itaendelea katika jimbo la Isimani kwa kumweka kitimoto mbunge wa jimbo hilo Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge, jimbo la Kalenga linaloongozwa na waziri wa Fedha Dkt Wiliam Mgimwa na jimbo la Kilolo linaloongozwa na Prof.Peter Msola na kuwaomba wabunge hao kushiriki midahalo hiyo.
Na francisgodwin.blogspot.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo