Makete
Wananchi wilayani Makete mkoani Iringa wamepongezwa kwa kuitikia na kuupokea mpango wa elimu ya watu wazima ujulikanao kama Intergrated Post Primary Education (IPPE)
Mratibu wa mpango wa IPPE taifa Bi Leonia Kassamia katika ziara ya kutembelea kituo kinachotoa elimu hiyo cha Itundu kilichopo shule ya sekondari Mlondwe wilayani hapa
Bi Kassamia amesema nia ya mpango huo ni kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu na kuongeza kuwa elimu ya watu wazima inatolewa kwa watu wote wenye uwezo wa kusoma na kuandika, masomo ambayo hufundishwa katika hatua tatu ambazo ni ufundi, taaluma pamoja na genetic
Kwa upande wao wanafunzi wa mpango huo wameiomba serikali kuendelea kuuboresha mpango huo kwani unaleta tija kubwa kwa wananchi
Wakati huo huo
Mratibu huyo wa IPPE Leonia Kassamia amewahimiza wananchi wa kata ya Iwawa wilayani Makete kujiunga katika mpango wa elimu ya watu wazima
Amezungumza hayo katika ziara ya kujifunza uanzishwaji wa kituo cha IPPE kayika kata hiyo kilichopo maeneo ya shule ya msingi Iwawa
Amesema wanafunzi walioshindwa mitihani yao kutumia fursa hii ya elimu ambayo itawasaidia kutambulika kwa kupata cheti mara baada ya kumaliza masomo ambapo watakuwa na uwezo wa kusoma hadi hatua ya shahada
Aidha amebainisha kuwa mfumo huu utapunguza mzigo kwenye familia kwani kila mtu atapata elimu na kufuta ujinga na utegemezi hivyo kuleta maendeleo katika jamii