Makete
Imeelezwa kuwa ukosefu wa gari kwa ajili ya kuzolea taka wilayani Makete ni moja ya sababu zinazopelekea mlundikano wa taka katika soko la wakulima Makete mjini
Hayo yamesemwa na Afisa Afya wa kata ya Iwawa wilayani hapa Bi. Agatha Mbilinyi wakati akizungumza na waandishi wetu kuhusiana na mlundikano wa taka sokoni hapo
Ameongeza kuwa ubovu wa barabara ya kuelekea lilipo dampo kwa ajili ya kupeleka taka hizo nayo imekuwa chanzo cha mlundikano huo wa taka katika soko hilo
Bi Mbilinyi amesema wakati mwingine wanalazimika kukodi gari la kubebea taka hizo kwa gharama zao wenyewe na wakati mwingine wamiliki wa magari hukataa kwenda kutokana na ubovu wa barabara ya kuelekea dampo hasa kipindi hiki cha masika
Aidha ameiomba halmashauri ya wilaya ya Makete kutenga gari maalum kwa ajili ya kubebea taka hizo kila mara pamoja na kuitengeneza barabara inayoelekea dampo