Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) Dr. Agnes Kijazi amesema kuanzia leo mvua zilizokuwa zikinyesha jijini DSM na kusababisha mafuriko zitaanza kupungua
Dr. Kijazi amewatoa hofu wakazi wa Dar kuwa mvua hizo zitaanza kupungua baada ya kunyesha kwa kiasi kikubwa kwa muda wa siku mbili mfululizo na kusema kuwa utabiri wao ulikuwa ni mvua kunyesha kwa siku mbili mfululizo, mvua ambazo zingekuwa na madhara makubwa
Wakati huo huo taarifa zilizotolewa na mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa kanda ya nyanda za juu kusini hususan mkoa wa Mbeya, mvua kubwa zitanyesha kati ya Disemba 21 - 31 mwaka huu na kusababisha madhara makubwa, hivyo wananchi wachukue tahadhari!