Shirilka la umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa hadi sasa ni mapema mno kuzungumzia hasara shirika hilo ilizozipata kutokana na miundo mbinu ya umeme kuharibiwa na mafuriko
Hayo yamesemwa na Meneja mahusiano wa shirika hilo Badra Masoud (pichani) wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya shirika hilo kulazimika kukata umeme kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ili kupunguza kutokea kwa madhara zaidi hususan vifo
Baadhi ya hasara shirika hilo ilizozipata ni pamoja na nguzo za umeme kuanguka, transfoma kuanguka pamoja na nyaya kukatika, ila amesema tathmini kamili ya hasara hizo itatolewa baadae na shirika hilo