Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick amesema hadi kufikia muda huu watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyolikumba jiji la Dar es Salaam kutokana na mvua iliyonyesha Desemba 21 mwaka huu imefikia 23
Akizungumza na mtandao huu mkuu huyo amesema hawana taarifa za kuongezeka kwa idadi ya marehemu na badala yake wanasubiria maji yakauke katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo kwani huenda miili mingine ikawa imenaswa kwenye tope la maji hayo
Aidha Sadick amewataka wakazi wa jiji la DSM kujitokeza kuitambua miili ya marehemu ambao bado hawajatambulika na kusema kuwa serikali ipo nao bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu zao kutokana na mafuriko hayo