Matokeo ya darasala 7 mwaka 2024 yametangazwa rasmi hii leo, ambapo unaweza kuyatazama kwa kubofya linki hapa chini
Bonyeza kwenye jina la shule husika kuona matokeo hayo
Unaweza kuangalia matokeo ya shule zote za msingi wilaya ya Makete mkoa wa Njombe kwa kubofya link hapa chini
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, amesema kuwa shughuli ya usimamizi na uratibu wa upatikanaji wa Katiba Mpya ya kisasa utasimamiwa na chama hicho na si vinginevyo.
Kijana Tyson Nduguru, Rafiki wa karibu wa Joel Misesemo (MC Joel) aliyejirusha ghorofa ya 7 Makumbusho Dar es salaam na kufariki dunia, ambaye aliripotiwa kutoweka ghafla siku tatu tangu kutokea kwa kifo cha Joel, amepatikana jana June 1 2023.
Baada ya kutolewa katazo la kutumia mazao yatokanayo na mnyama aina ya Nguruwe wilayani Ludewa mkoani Njombe ambalo lilitolewa kwa zaidi ya miezi miwili na nusu iliyopita kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na uwepo wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe hatimaye mnyama huyo ameweza kupunguziwa masharti ya katazo hilo baada ya kupungua kwa matukio ya ugonjwa huo.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Mbeya vijijini kimetangaza kumfutia uanachama Joseph Mwasote ‘China wa China’ ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mbeya akidaiwa kuwa chanzo cha migogoro ndani ya chama hicho.
Tume ya Haki za Binadamu (THBUB) imetoa matokeo ya uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Nusura Abdallah, huku ikidai hakikuwa na uhusiano wowote na ajali ya Naibu Waziri Dk Festo Dugange iliyotokea Aprili 25 kuamkia 26 mwaka huu.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 40 kutoka nchini Zambia, Arnold Masuka, ameiomba mahakama kuvunja ndoa yake kutokana na urembo wa kipekee alionao mke wake.
Masuka aliwashangaza viongozi na mashahidi katika mahakama ya mji mkuu wa Lusaka wakati alipomwambia hakimu kwamba urembo wa mkewe, Hilda Mleya umemfanya kukosa usingizi mara kadhaa.
Mzaliwa huyo wa Lusaka ameongeza kuwa amekuwa akiishi kwa hofu kwa muda mrefu ya kumpoteza mke wake kwa mwanamume mwingine, na hata anahofia kumuacha mke wake nyumbani peke yake anapotaka kwenda kazini kwa kuogopa huenda akashawishiwa na wanaume wengine.
Mwanaume huyo amemtaja mke wake, Hilda anayetokea Gokwe nchini Zimbabwe, kuwa ndiye mwanamke mrembo zaidi aliyewahi kukutana naye.
Katika mazungumzo na wanahabari baada ya kesi hiyo, Karani wa mahakama hiyo, Chenjerai Chireya amekiri kwamba hajawahi kushuhudia tukio kama hilo mahakamani katika miaka yake yote ya utumishi.
Na David John, Tanga
WANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki katika mbio za Mamathon ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo zilizoandaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo.
Lengo la kufanyika kwa Mamathon ni kutoa hamasa kwa wanawake wajawazito kujifungua salama na hatimaye kupunguza vifo vya mama na mtoto kama ambavyo Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
Akizungumza mbele ya wanawake hao, wananchi pamoja na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Wilaya ya Korogwe , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mary Chatanda aliyekuwa mgeni rasmi amempongeza Jokate kwa ubunifu huo.
“Tunakupongeza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo kwa kazi kubwa ambayo anaifanya na kote alikopita amekuwa akifanya kazi nzuri hivyo wananchi wa Wilaya ya Korogwe wajue wamepata jembe na ndio maana Rais Dkt Samia Hassan Suluhu ameendeea kumteua katika nafasi hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe .
“Wananchi wa Korogwe mmepata jembe na muendelee kumpa ushirikiano na sisi viongozi tutaendelea kumuunga mkono na katika hili la ambalo ameliazisha aendelee nalo kwani linagusa maisha ya wamama wajawazito na watoto moja kwa moja kulinda afya zao, ” amesema Chatanda.
Pia amewataka wananchi wa Korogwe kumtumia Mkuu wa Wilaya hiyo kwani ana mambo mazuri yatakayowezesha kuwaletea maendeleo na wao kama viongozi wa Chama na Serikali watatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anatekeleza majukumu yake vizuri.
Akifafanua kuhusu mbio za Mamathon amesema ni jambo jipya katika Wilaya ya Korogwe na Jokate ameonesha ubunifu mkubwa, hivyo anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mkuu huyo wa Wilaya kwani mambo yamekuwa moto.
amewapongeza wanawake wajawazito pamoja na wote walioshiriki na kumaliza mbio hizo kwani kufanya mazoezi kwa mjazito kuna faida nyingi.”Kupitia mbio hizi kuna mama mjamzito mmoja amepelekwa hospitali na tunamuombea ajifungue salama.”
Amewataka kuhakikisha baada ya mbio hizo wanaendelea kushiriki mazoezi ,kuzingatia lishe Bora kipindi chote cha ujauzito wao jambo litakalosaidia kujifungua salama na kuwezesha mpango wa Serikali wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.
Pamoja na mambo mengine Chatanda amesema mbali ya mbio hizo, amepokea vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Korogwe na hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuboresha huduma za afya ikiwemo ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
“Kuna kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt Samia Kwa kazi kubwa anayoifanya katika sekta ya afya na kwa kipindi cha miaka miwili kwa nchi nzima ameboresha miundombinu kwenye sekta ya afya katika ngazi zote za Zahanati ,vituo vya afya ,Hospitali za Wilaya , na kungineko na kupeleka vifaa tiba Kwa ajili ya kutolea huduma za afya.”
Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wahudumu katika vituo vya afya Zahanati ,na Hospitali zote kuzingatia maadili ya kazi zao, na kuepuka na vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kazi wanayoifanya huko akitolea mfano vitendo vilivyojitokeza wilayani Kaliua mkoani Tabora na anashukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora Baltida Burhan kwa kuchukua hatua.
Kenny na Lenny Makomonde (24), mapacha na wanafunzi wa Chuo cha Mipango Kampasi ya Mwanza wamefariki dunia kwa kuzama majini walipokuwa wakiogelea ndani ya Ziwa Victoria.
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema takribani nusu ya miradi ya kimkakati iliyoainishwa na serikali ipo kwenye sekta ya nishati.