Ndoa ya Haji Manara na Wema Sepetu yaota mbawa

Ni kama ndoa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wengi kati ya Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara na mlimbwende Wema Sepetu imeota mbawa baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupangua tena ratiba ya ligi kuu kwa kusogeza mbele mchezo wa Azam na Ndanda FC.
Mchezo huo uliokuwa umepangwa kufanyika Jumamosi ya Februari 4, sasa utafanyika Jumapili Februari 5 ili kutoa nafasi kwa Azam FC kujiandaa vizuri kutokana na timu hiyo kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, siku ya Jumatano usiku.
Maamuzi haya yamefanyika ikiwa ni takriban siku 10 tangu Haji Manara atangaze kumposa aliyewahi kuwa Miss Tanzania, ambaye pia ni malkia wa filamu hapa nchini Wema Sepetu endapo ratiba isingepanguliwa tena.
Manara amesema alikuwa na uhakika kuwa ni lazima ratiba ingepanguliwa tena, mara baada ya TFF pia kupangua tarehe ya mchezo kati ya Simba na Yanga uliosogezwa kutoka Februari 18 hadi Februari 25 huku akionesha kushangazwa na jinsi ambavyo TFF inashindwa kutengeneza ratiba ya uhakika.
Katika taarifa yake aliyoitoa usiku wa Januari 23 mwaka huu, Manara alisema  “Iwapo Kama ratiba yao ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka nyumbani kwangu hadi TFF”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo