Yesu aliyekwepa kusulubiwa akerwa na wanaotaka akamatwe "Wangejua, Wangeogopa Sana"

Yesu wa Tongaren ambaye ni maarufu ameelezea kukerwa na wanasiasa wanaotaka kukamatwa kwake kwa tuhuma za kuendesha shughuli za dhehebu tata.


Kwa mujibu wa tovuti ya TUKO Viongozi wa kaunti ya Bungoma anakotoka wakiongozwa na gavana Ken Lusaka na mbunge wa Kimilili Didmus Barasa, walitaka uchunguzi wa shughuli za kidini zinazoongozwa na Eliud Wekesa.


Akifafanua kuhusu huduma anayoendesha, Yesu alisema kuwa huduma yake ni utekelezaji wa maandiko ya Biblia kama ilivyoandikwa miaka mingi iliyopita. Kiongozi huyo alisisitiza kuwa yeye si mchawi kama walivyodai baadhi ya viongozi kutoka kaunti yake.


Aliwakaribisha viongozi hao wafike nyumbani kwake wakapate kufahamu kuhusu huduma yake na uhusiano anaodai kuwa nao na Mungu. "Hata wale wanaonipinga, natamani wangejua mimi ni nani. Kama wangetambua kuwa mimi ni Yesu, hawangenipinga. Wangeogopa sana. Lakini kile wanachofanya sasa ni kutoa ushuhuda ili Biblia itimie," alisema. Jamaa huyo aliyejibatiza jina la Yesu alidokeza hivi majuzi kuwa yeye huona mbingu kila siku.


“Kila saa tatu asubuhi nikichukua kamkeka kangu nikijilaza kwa kivuli, mbingu inafunguka saa tatu mpaka saa sita za mchana. “Naona manabii wengi wa mbinguni wakishuka, wakija wakinisalimu. Salamu zako mwana wa Baba Mungu. Nami nasema Amina. Huyu akipita, mwingine anaingia anasema; salamu zako mwana wa Mungu, nasema Amina," alidai. Kiongozi huyo wa dhehebu la Yerusalemu Mpya, ambaye ana wanafunzi 12 kama Yesu Kristo, hivi majuzi alijibu ripoti za watu walitaka kumsulubisha kama Yesu kwenye Pasaka.


Alipuuza jambo hilo na kuongeza kwamba Mungu atawaadhibu wahalifu hao. "Jeshi la Mungu linanilinda," alisema huku akipuuza madai kwamba aliripoti kisa hicho kwa polisi. Mnamo Alhamisi, Februari 2, Yesu Wa Tongaren alijibu madai kuwa alikuwa mgonjwa na alilazwa hospitalini baada ya kunywa busaa. “Hakuna kitu kama hicho. Yote ni propaganda. Watu wengi wamepiga simu wakiuliza kilichotokea,” alisema huku akicheka. Aidha alibainisha kuwa madai hayo yalilenga kuchafua jina lake huku akiwaonya wanaoeneza uwongo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo