Pasta Ezekiel Odero Aitaka Mahakama Kulifungua Kanisa Lake

Mmiliki wa kanisa la New Life Prayer Centre Mchungaji Ezekiel Ombok Odero amewasilisha ombi katika mahakama kuu ya Mombasa akitaka kufunguliwa kwa kanisa lake lililofungwa Mavueni, Kaunti ya Kilifi.


Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini Kenya inasema, Kupitia wakili Danstan Omari, Ezekiel aliwasilisha ombi hilo akiteta kuwa haki ya waumini wake ya kuabudu ilikiukwa baada ya kanisa hilo kufungwa. 


Katika hati zilizowasilishwa kortini, Kamishna wa ukanda wa Pwani Rhoda Onyancha alitajwa kuwa aliyetangaza kufungwa kwa kanisa hilo hadi itakapotangazwa tena katika mkutano na wanahabari.


Omari aliteta kuwa Onyancha alifaa kungoja matokeo ya maombi mengine tofauti mbele ya mahakama kabla ya kufanya uamuzi wa kufunga kanisa hilo.


“Baada ya tamko la Onyancha, mteja wangu mnamo Aprili, 27 alipokea barua kutoka kwa Bw. Ezra Chiloba Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya, akiwasilisha uamuzi wa mamlaka ya kusimamisha kwa muda shughuli/masafa ya Televisheni ya Uinjilisti ya Dunia ambayo ni. inayoendeshwa na mwombaji kama chombo cha kisasa cha kueneza huduma na injili,” alibainisha.


Omari alidai kuwa tuhuma zinazomkabili Ezekiel hazina uthibitisho, niza ki kashfa na si za kweli. Aliongeza kuwa kumekuwapo na ongezeko la ushinikizaji kutoka upande wa walioshtaki ambao kwa sasa wanatishia kufungia akaunti za benki za kanisa hilo kwa nia ovu ya kudumaza shughuli zote za mshtakiwa na kanisa la New Life Prayer Center. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo