Polisi wakamata watu 56 wakielekea kwenye maombi

Jeshi la Polisi katika kaunti ya Nakuru huko nchini Kenyawamewakamata takriban raia 56 wa Uganda ambao wanadaiwa walikuwa safarini kuelekea Ethiopia kwa ajili ya maombi.


Nation inaripoti kuwa Waganda hao ambapo watu wazima walikuwa 29 na watoto 27 wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na mitano walikamatwa katika kituo cha basi mjini Nakuru kwa kukosa stakabadhi za kusafiria.


Abiria hao walikuwa wamesimama kupata viburudisho mjini humo wakati mwananchi aliyekuwa na shaka aliposhtushwa na wingi wao na kuwadokeza polisi.


Naibu Kamishna wa Kaunti ndogo ya Nakuru Mashariki Were Simiyu alisema: “Wananchi hao wa Uganda hawakuwa na hati za kusafiria kuonyesha walikuwa hapa kihalali. Wanachukuliwa kuwa wahamiaji haramu. Walisema walikuwa wakielekea Ethiopia kwa maombi."


Raia hao walitoroka kisiri kutoka wilaya ya Ngora, Mashariki mwa Uganda kupitia kwa mpaka wa Kenya na Uganda, Busia. Kulingana na Simiyu, wageni hao 56 watarejeshwa nchini mwao ili kupata hati sahihi za kusafiria kabla ya kuendelea na safari yao ya kuelekea Ethiopia. "Tumeamua kuwa kwa sababu hawa ni marafiki zetu kutoka nchi jirani na hawana hati stahili za kusafiria, tutawarudisha nchini mwao ili waweze kupanga safari zao upya," aliongeza Simuyu.


DCI waanza upelelezi Maafisa wa upelelezi wameanzisha uchunguzi kumtambua pasta huyo ili kumhoji. Isaac Adile, 27, mkazi wa kijiji cha Ommo nchini Uganda, alisema kuwa wao ni waumini wa Kanisa la Christ Disciples Church (CDC) linaloongozwa na kiongozi wao wa maombi aliyetambulika kama Isaac Omiata. Alisema kuwa walikuwa wakienda kwa kongamano la wiki moja la kanisa katika tawi lao la kanisa nchini Ethiopia. 


Chanzo:tukokiswahili


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo