Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Majaji kufanya kazi bila kuwa na upendeleo katika maamuzi yao, hasa kwenye kesi zinazowakabili Wafugaji na maeneo ya hifadhi.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akiwaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu mkoani Dodoma.
“Nimpongeze Jaji Mkuu kwa kupata timu mpya. Unajua katika ripoti zetu na hasa tukienda nje, Tanzania tunapata "credit" kwani wastani wa Majaji kwenye Mahakama ya Rufani 47 kwa 50 na wanakaribia 50-50.
Kwa hiyo kila nikitengeneza jopo nitakulete na Wanawake ili nifikie 50-50 jambo ambalo hatukulizoea huko nyuma.
Lakini sasa sababu Wanawake wapo na "wana-qualify", na nina hakika Majaji Wanawake ni wazuri zaidi na huwa wanaogopa dhambi zaidi.” -Rais Samia Suluhu Hassan